AMMAN-Iraq na Jordan zarejesha nyumbaniwawakilishi wao katika nchi hizo.
21 Machi 2005Iraq na Jordan kila moja imemrejesha nyumbani mwakilishi wake katika nchi hizo.Hiyo ni hatua ya hivi karibuni kabisa kuchukuliwa na nchi hizo mbili,baada ya kuwepo kauli za kuishutumu Jordan kuwa inawaunga mkono waasi wanaoedesha upinzani nchini Iraq.Serikali ya Jordan imesema balozi wake mdogo aliyekuwa nchini Iraq amerejeshwa mjini Amman kwa mashauriano zaidi.Baada ya taarifa hiyo msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iraq mjini Baghdad alitoa taarifa ya kuitwa nyumbani kwa mwakilishi wao aliyepo mjini Amman.
Kumekuwa na vitendo vya upinzani dhidi ya Jordan katika kipindi cha wiki moja iliyopita.Upinzani huo umeibuka baada ya kuwepo ripoti kuwa raia wa Jordan ndie aliyehusika na kujitoa muhanga katika shambulio lililosababisha kuuawa kwa watu 125 kusini mwa Baghdad mwezi uliopita wa Februari.
Hata hivyo serikali ya Jordan pamoja na familia ya mtu huyo,wamekanusha kuhusika kwa mtu huyo katika shambulio hilo.