Kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso amethibitisha, ataondoka Bay Arena mwishoni mwa msimu huu. Anatazamiwa kujiunga na miamba wa Uhispania Real Madrid. Alonso amesema huu ndio wakati sahihi wa kutangaza kuondoka kwake. Alikuwa na kandarasi hadi 2026 lakini klabu hiyo ilisema imekubali matakwa yake ya kusitisha mkataba wake mwishoni mwa msimu.