MigogoroMarekani
Aliyewaua watumishi wa ubalozi ashitakiwa kwa mauaji
23 Mei 2025Matangazo
Rodriguez, mzaliwa wa Chicago anatuhumiwa kwa kuwafyatulia risasi watu walipokuwa wakiondoka kwenye hafla iliyowakutanisha wataalamu chipukizi na wanadiplomasia, iliyoandaliwa na Kundi la Wayahudi linalopambana na chuki dhidi yao.
Kulingana na nyaraka za mashitaka, Rodriguez aliwaambia polisi kwenye eneo la tukio kwamba alifanya hivyo kwa ajili ya Wapalestina na Gaza.
Waliouawa kwenye tukio hilo la Jumatano usiku ni Yaron Lischinsky na Sarah Lynn Milgrim, ambao walikuwa mbioni kufunga ndoa.