Charles Hillary afariki dunia
11 Mei 2025Matangazo
Msemaji mkuu wa serikali na mkurugenzi wa habari na mawasiliano ya rais wa Zanzibar, Charles Hillary amefariki dunia, leo Jumapili jijini Daresalam. Charles Hillary aliyezaliwa Oktoba mwaka 1959, aliwahi kufanya kazi na mashirika kadhaa ya habari ya Kimataifa ikiwemo Idhaa hii ya Kiswahili ya DW,Ujerumani ambako alifanya kazi kama mtangazaji na mhariri kwa takriban miaka minne mjini Bonn. Dw Kiswahili Inatowa pole kwa familia, jamaa na marafiki wa nguli huyu wa tasnia ya habari,tangu mwaka 1980, mchango wake utakumbukwa daima.