Mshambuliaji Soko la Krismasi Magdeburg ashtakiwa kwa mauaji
19 Agosti 2025Matangazo
Mshtakiwa huyo alilivurumisha gari lake kwenye umati wa watu mnamo Desemba mwaka 2024.
Mtuhumiwa huyo aliyetambuliwa kama Taleb A, mwenye umri wa miaka 50, anakabiliwa na mashtaka sita ya mauaji na jaribio la kuwaua watu 338, miongoni mwa mashtaka megine.
Wanawake watano waliokuwa na umri wa miaka 45 hadi 75 na mvulana mwenye miaka 9 waliuawa katika shambulizi hilo.
Maafisa wamesema shambulizi hilo lilidumu kwa zaidi ya dakika moja, huku gari lake likiwa na kasi ya kilomita 48 kwa saa.
Bado haijafahamika ni lini kesi hiyo itaanza kusikilizwa.
Mahakama ya muda inajengwa huko Magdeburg na inatarajiwa kukamilika mwezi Septemba.
Mshtakiwa anaendelea kushikiliwa rumande.