Nchi 3 za Afrika zasaini mkataba wa bomba la gesi asilia
12 Februari 2025Maafisa kutoka Algeria, Nigeria na Niger wametia saini mikataba mipya inayolenga kuharakisha uendelezaji wa bomba kubwa la gesi asilia kuelekea Ulaya.
Bomba hilo la gesi lililotangazwa mwaka 2009, litasafirisha mabilioni ya mita za ujazo za gesi kutoka Nigeria kupitia Niger hadi Algeria. Kutoka hapo gesi hiyo itaweza kusafirishwa kupitia bomba la chini ya bahari kwenda Italia, au kupakiwa kwenye meli za gesi asilia zilizowekwa kimiminika kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi. Kwa nini gesi asilia bado inatiririka kutoka Urusi kwenda Ulaya kupitia Ukraine?
Nchi hizo tatu zilitia saini mikataba kuhusu ripoti ya upembuzi yakinifu na masuala mengine, ikiwa ni pamoja na makubaliano nyeti kati ya makampuni ya nishati ya serikali.
Mradi huo umepewa msukumo kutokana na ongezeko la mahitaji ya gesi na kupanda kwa bei ulimwenguni kote kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.