ALEXANDRIA: Mtu mmoja auwawa katika maandamano nchini Misri
22 Oktoba 2005Matangazo
Mtu mmoja ameuwawa kwenye maandamano mjini Alexandria nchini Misri ya kupinga mchezo wa kuigiza ambao waandamanaji wanasema unaoidhalilisha dini ya kiislamu. Maofisa wa serikali wamesema mtu huyo aliuwawa wakati wa mapigano kati ya waandamanaji takriban elfu tano na maofisa wa polisi.
Watu wengine wengi wakiwemo polisi walijeruhiwa katika vurumai hizo, zilozofanyika nje ya kanisa ambamo mchezo huo ulionyeshwa. Mchezo huo unahusu mwanafunzi wa kikristo katika chuo kikuu anayekubali kusilimu na kuwa muislamu baada ya wanaume wa kiislamu kumuadi kumpatia fedha.