MigogoroMashariki ya Kati
Albanese: Mataifa yakomeshe "mauaji ya halaiki" Gaza
16 Julai 2025Matangazo
Afisa huyo, Francesca Albanese, anayeshughulikia Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi, ametoa matamshi hayo alipokuwa akizungumza na wajumbe kutoka nchi 30 waliokusanyika kwenye mji mkuu wa Colombia, Bogota kujadili vita vinavyoendelea kati ya Israel na kundi la Hamas.
Wajumbe hao wanatafuta njia ambazo mataifa duniani yanaweza kutumia kukomesha mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza. Kwenye hotuba yake Albanese amesema nchi duniani zinapaswa kupitia upya ushirikiano wao na Israel na kusitisha mara moja mahusiano na taifa hilo.
Israel imekanusha mara kadhaa madai kuwa inafanya "mauaji ya halaiki" kwenye mzozo wa Ukanda wa Gaza ambao tayari umesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 50,000.