Al-Sisi kutohuhudhuria mkutano wa Trump kuhusu Gaza
12 Februari 2025Taarifa kutoka vyanzo viwili va usalama zimesema Marekani ilipeleka mwaliko kwa Sisi kuzuru White House mapema mwezi huu, ingawa kulingana na afisa mmoja bado hakujatajwa tarehe rasmi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdelatty alizuru Washington wiki hii, na vyanzo ya Misri vilisema lengo mojawapo la ziara hiyo lilikuwa ni kuepusha ziara ya rais ambayo ingeweza kusababisha utata.
Soma pia:al-Sisi asema hatozungumza na Trump kuhusu mpango wa Gaza
Kulingana na vyanzo hivyo, Abdelatty alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, alielezwa wazi kwamba suala hilo la kuwahamisha Wapalestina litajadiliwa kwenye ziara hiyo ya Sisi.
Ofisi ya rais wa Misri pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje hata hivyo haikuzungumzia taarifa hiyo ilipoombwa kufanya hivyo.