al-Sisi amhimiza Trump kumaliza vita vya Gaza
28 Julai 2025Matangazo
Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni, Sisi amesema kuwa Trump ndiye mwenye uwezo wa kusimamisha vita, kuleta misaada na kumaliza mateso katika eneo hilo katika wakati ambapo wakazi wa Gaza wanakabiliana na hali mbaya ya kibinadamu.
Al-Sisi kutohuhudhuria mkutano wa White House kuhusu uhamisho wa watu wa Gaza
Rais huyo ambaye serikali yake imehusika katika juhudi za upatanishi zilizolenga kusitisha mapigano pamoja na kuruhusu kuingizwa kwa msaada katika ukanda wa Gaza, amesema kuwa wakati umewadia wa kumaliza vita hivyo.
Wakati huo huo, Rais Trump amesema leo kuwa usitishaji vita kati ya Israel na Hamas bado unawezekana baada ya mazungumzo mjini Doha kwa usimamizi wa Marekani, Qatar na Misri kumalizika bila mafanikio.