Madhila makubwa yawapatayo wanaoishi na Virusi Vinavyosababisha Ukimwi (VVU) ni kubaguliwa na jamii, ambako huumiza zaidi kuliko hata ugonjwa wenyewe. Nchini Rwanda, mwanamke mmoja ameamua kuwasaidia kupambana nalo.
Sylvanus Karemera anazungumzia namna mwanamke shupavu nchini Rwanda anavyovunja kuta za ubaguzi dhidi ya wale wanaoishi na VVU na kuwapatia fursa za ajira kwenye kilimo cha uyoga.