Afrika Kusini yatangaza mgao wa umeme wa nchi nzima
23 Februari 2025Matangazo
Afrika Kusini imekumbwa na tatizo la kukatika ghafla kwa umeme katika maeneo mengi ya nchi leo Jumapili huku shirika la taifa la umeme Eskom likitangaza mgao wa umeme katika taifa hilo lililostawi zaidi kiviwanda barani Afrika.
Tangazo hilo limekuja kwa mshangao baada ya taarifa ya kutia moyo kutoka kwa shirika la Eskom kwamba tatizo la miaka mingi la kukatika kwa umeme wakati mwingine hadi saa 12 kwa siku linaweza kumalizika hivi karibuni.
Soma: Janga la kitaifa latangazwa Afrika Kusini kufuatia ukosefu wa umeme
Shirika la taifa la umeme lenye deni kubwa lilisema katika taarifa yake kuwa linalazimika kufanya mgao wa umeme kwa muda usiojulikana kwa sababu ya hitilafu nyingi katika mitambo mitatu ya nishati ya makaa ya mawe.