MigogoroAfrika Kusini
A. Kusini yataka Ukraine kushirikishwa mazungumzo ya amani
22 Februari 2025Matangazo
Vita hivyo vilikuwa mada kuu katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la G20 nchini Afrika Kusini uliomalizika jana Ijumaa.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kufanya ziara ya kiserikali hivi karibuni nchini Afrika Kusini kufuatia mwaliko wa Rais Cyril Ramaphosa kujadili usitishaji vita.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Ronald Lamola amewaambia waandishi wa habari kwenye mkutano wa mwisho baina yao kwamba mazungumzo hayo yalikuwa na tija kubwa na kuongeza kuwa yalitambua "ongezeko la mgawanyiko wa siasa za maeneo" limechangia "hali ya kutoaminiana".