Afrika Kusini kukutana na Misri katika AFCON
28 Januari 2025Wenyeji Morocco wataangushana na Comoro katika mechi ya ufunguzi ya mashindano hayo yenye timu 24 mnamo Desemba 21. Mabingwa watetezi Ivory Coast watakutana na washindi mara tano Cameroon katika Kundi F ambalo pia lina Gabon na Msumbiji.
Sudan imepangwa na Algeria, huku mtanange kati ya Senegal na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ukiipamba hatua ya makundi. Kando na Afrika Kusini, Misri, washindi mara saba watacheza dhidi ya Angola na Zimbabwe katika Kundi B.
Soma pia:Nigeria yawaondoa Afrika Kusini na kutinga fainali za AFCON
Majirani Uganda na Tanzania wanakamilisha Kundi C pamoja na Nigeria na Tunisia. Kuandaa michuano ya AFCON kunaonekana kuwa sehemu muhimu ya matayarisho ya Morocco kuelekea Kombe la Dunia la mwaka 2030, ambalo taifa hilo la Kifalme litaandaa kwa pamoja na Uhispania na Ureno.