Afrika kupata nishati ya uhakika kufikia 2030
28 Januari 2025Azimio lililoweka ahadi zao za kuhakikisha kuna mabadiliko ya kisera, kisheria na mipango itakayowezesha upatikanaji wa uhakika wa nishati katika nchi za Afrika.
Marais na wakuu wa nchi za Afrika, kusaini azimio la Dar es salaam ambalo limejikita katika kuhakikisha watu milioni 300 katika nchi za Afrika wanapata umeme ifikapo mwaka 2030 leo Januari 28.
Mpango huo unalenga kuwekeza angalau dola bilioni 90 za mtaji kutoka benki za maendeleo ya kimataifa, mashirika ya maendeleo, taasisi za kifedha, wafanyabiashara binafsi, na mashirika ya kifedha ya hisani, kulingana na Wakfu wa Rockefeller, ambao ni sehemu ya mpango huo.
Aliyesoma azimio hilo lenye maazimio 15 kwa niaba ya marais na wakuu wa nchi Afrika ni Katibu Mkuu wa Benki ya Maendeleo Afrika, (AfDB) Profesa Vicent O Nmehielle.
Miongoni mwa maazimio hayo ni pamoja na Kutekeleza mpango wa upatikanaji wa umeme na nishati safi ya kupikia, Kuimarisha na kuboresha miundombinu ya umeme na kufikisha umeme kwa wateja kwa kutumia mifumo nafuu na wala sio kwa kutegemea rasilimali za ndani pekee.
Soma pia:Mataifa ya Afrika yanatafuta namna ya kuwaunganisha watu milioni 300 ifikapo 2030
Mengine ni kuwekeza katika njia tofauti za kuzalisha umeme ikiwamo umeme wa jua, maji na jotoridi?? na Kutengeneza mazingira wezeshi kwa kuwa na sera na mipango rafiki ya kuzalisha umeme na kuwa mifumo shindanishi ya manunuzi ya rasilimali za nishati.
Baada ya kusomwa kwa maazimio hayo, baadhi ya wakuu wa nchi waliahidi mbele ya hadhara hiyo wanakwenda kufanya nini katika nchi zao ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa umeme.
Somalia: Tunaboresha taasisi zetu za umeme
Kwa upande wake, Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Muhamud, alisema Somalia inaanzisha na kuboresha taasisi za umeme kwa kuhakikisha kuna mifmo bora ya kuvutia wawekezaji.
Awali, akifungua mkutano huo, Rais Samia Suluhu Hassan alisema, Tanzania inajipanga kufanya mambo manne ili kuondokana na changamoto ya nishati ikiwa ni pamoja na kuwezesha biashara ya umeme miongoni mwa nchi za Afrika, kufikisha umeme katika vitongozi vya Tanzania, kupitia mpango huo.
Soma pia:Uzalishaji wa mafuta ya visukuku waongezeka mwaka 2024, tathmini ya mwaka yaonyesha
Bara la Afrika lina idadi kubwa zaidi ya watu wasio na upatikanaji wa umeme ulimwenguni na linakimbizana kufikisha huduma hiyo katika majumba ifikapo mwaka 2030 chini ya mpango uliopewa jina la "Mission 300," uliozinduliwa na Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) mwezi Aprili.