Magazeti ya Ujerumani yameangazia maafa yaliyotokea nchini Afrika kusini, vuta nikuvute nchini Angola juu ya mazishi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Eduardo dos Santos aliyefariki nchini Uhispania mapema mwezi huu, mjadala unaohusu njia ya ufanisi ya kulinda usalama wa wananchi nchini Nigeria miongoni mwa maudhui mengine. Mtayarishaji ni Zainab Aziz.