Afrika katika magazeti ya Ujerumani tarehe 11-03-2005
11 Machi 2005Tamasha la filamu za Afrika linalofanyikia mjini Ouagadougou Burkina-Faso kila baada ya miaka miwili hujishughulisha na utengenezaji wa filamu, lakini kazi nyingine muhimu ya tamasha hili linalozidi kuwa na mafanikio, ni mikakati ya kusambaza filamu nzuri za Afrika duniani kote.
Gazeti la NEUES DEUTSCHLAND limeandika makala ndefu kuhusu mada hii:
"Katikati ya mji wa Ouagadougou kumewekwa mnara wa kuenzi kazi za watayarishaji wa filamu. Huu ni mji pekee barani Afrika kutoa naafasi kama hii ya kuonyesha umuhimu wa kazi za watengenezaji wa filamu.
Tangu mwaka 1969, nchi ndogo ya Burkina Faso iliyo na eneo la kilometa za mraba 300,000 huandaa tamasha maalumu la filamu za Afrika, lijulikanalo kwa jina la FESPACO. Muda mfupi baada ya nchi hii ya Afrika Magharibi kujinyakulia uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Ufaransa, majumba yote ya filamu yalitaifishwa. Asilimia 15 ya mapato yaliyokuwa yanapatikana kwa kuazimisha filanu za kigeni, ikawa inatumiwa kwa ajili ya kuendeleza sekta ya kutengeneza filamu ndani ya nchi. Kwa kutoka na pesa hizi mfuko maalumu ulianzisha na majumba kadha-wa-kadha ya kuonyeshea filamu yakajengwa, hali kadhalika kituo cha kuhifadhi filamu za Afrika.
Kila baada ya miaka miwili, kuanzia mwaka 1969, watengeneza filamu, wacheza filamu na wasimamizi wa shughuli hii, kutoka nchi mbalimbali za Afrika hufika kwenye maonyesho haya. Tamasha linaloambatana na burudani ya muziki na ngoma za kienyeji, limepanuka sana na hivi sasa linawavutia pia waandishi wa habari na watalii wengi kutoka duniani kote.
Wakati tamasha hili linaendelea kutafuta njia za kusambaza filamu za waafrika katika nchi za mbali, tatizo linabaki kuwa, gharama za kuangalia filamu katika nchi za Afrika bado ziko juu. Teknolojia ya kutumia DVD-Player na Video Beamer inapunguza gharama hii kwa kiasi fulani."
Hayo yameandikwa kwenye gazeti la NEUES DEUTSCHLAND.
Viongozi wa Uingereza, waziri mkuu Tony Blair na waziri wa fedha Gordn Brown, wametoa pendekezo kabambe la namna ya kuzisadia nchi maskini barani Afrika kwa kiwango kikubwa. Mpango huu unazitaka nchi za viwanda zitoe mabilioni ya fedha kwenye mfuko maalumu kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Lakini wasiwasi unazidi kuongezeka kuhusiana na utekelezaji wa mpango huu.
Gazeti la FINANCILA TIMES hapa Ujerumani limeandika:
"Mpango huu wa Uingereza uliopokewa kwa shangwe unaelekea kukwama kwani benki kuu na wataalamu wa takwimu wa nchi za Ulaya wanataka marekebisho ya kina kwenye mpango. Wanataka fedha zinazotolewa chini ya mpango huu zipitie kwenye mifuko ya serikali husika.
Hata kuchelewa kwa mfuko husianifu wa kimataifa IFF kuwasiliana na taasis ya takwimu ya Umoja wa Ulaya nako kunachangia kwenye utata huu. Kwa mujibu wa pendekezo la Uingereza, mfuko huu ungeanza kutumiwa mara moja, kabla hata ya kuanza kuongoza kundi la nchi 7 zinazoongoza kiuchumi duniani.
Mpango huu umeanza kukosolewa na walengwa pia; kwa mfano waziri mkuu wa Msumbiji LULSA DIAS DIOGO, amenukuliwa akisema, mpango huu hautakuwa na mafanikio iwapo hautaboresha uwezo wa nchi za Afrika kuuza bidhaa zake kwenye masoko ya kimataifa.
Marekani na Canada na benki kuu katika baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya zinakosoa pia baadhi ya vipengee vya mpango huu. Hoja inayotolewa, kwa mfano na Ujerumani ni kutohusishwa kwa msaada huu na masuala ya bajeti ya nchi husika, kwani unaweza kuongeza matumizi kinyume na kanuni za uthabiti wa Euro."
Hayo yameandikwa kwenye gazeti la Ujerumani la FINANCIAL TIMES.
Nalo gazeti la TAZ limeandika juu ya ongezeko la kasi la matumizi ya simu za mkononi barani Afrika.
"Soko la simu za mkononi katika kontinenti la Afrika ndiyo linaloongoza kwa kustawi kwa kasi duniani kote. Kauli hii inatokana na matokeo ya utafiti uliofanywa na kituo cha utafiti wa masuala ya uchumi nchini Uingereza, CEPR, kwa ajili ya shirika kubwa la simu za mkononi VODAFONE.
Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huu, tangu mwaka 1998 hadi mwaka 2003, simu za mkononi zimeongezeka barani Afrika kwa asilimia 5,000. Zaidi ya hapo, utafiti huu umedhihirisha kwa mara ya kwanza uhusiano wa ongezeko la simu za mkononi na maendeleo ya kiuchumi. Simu za mkononi zimeleza mabadiliko makubwa kwenye teknolojia ya mawasiliano ya simu.
Gharama za simu hizi bado ziko juu na ndiyo maana baadhi ya watu barani Afrika wanatumia simu moja, kwa mfano nchini Tanzania, watumiaji wa simu ni mara dufu ya idadi ya simu za mkononi nchini humo.
Hata hivyo bado kuna njia ndefu, wakati Afrika nzima ina watumiaji wa simu za mkononi takribani milioni 82, Ujerumani peke yake kuna zaidi ya watumiaji wa simu hizi milioni 65.