SiasaUrusi
Afisa: Kombora lilitumika kushambulia jengo la serikali Kyiv
9 Septemba 2025Matangazo
Mkuu wa utawala wa rais, Andriy Yermak, amesema shambulio hilo la Jumapili lilikuwa la kwanza la aina hiyo tangu vita kuanza zaidi ya miaka mitatu iliyopita, na kwamba kombora la Iskander ndilo lililotumika.
Shambulio hilo lilikuwa sehemu ya wimbi kubwa zaidi la droni na makombora tangu Februari 2022. Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Ukraine, Katarina Mathernova, aliyetembelea eneo hilo, amesema jengo lingeharibiwa kabisa iwapo kombora hilo lingelipuka kikamilifu.
Takriban mita za mraba 900 za jengo hilo zimeathirika, huku moto mkubwa ukienea kwa kasi.
Ukraine sasa inatoa wito kwa washirika wake kuongeza vikwazo dhidi ya Moscow, baada ya shambulio hilo kuua na kujeruhi watu kadhaa.