Ujerumani yaiorodhesha AfD kuwa taasisi yenye itikadi kali
2 Mei 2025Hatua hiyo inalipa uwezo zaidi shirika hilo kukifuatilia kwa karibu chama hicho kilichoshika nafasi ya pili katika uchaguzi wa kitaifa uliofanyika mwezi Februari.
Pia itazirahishia zaidi mamlaka za Ujerumani kutumia njia za siri kama vile kuwapenyeza watu wake katika kulichunguza na kufuatilia mawasiliano yake. Itakumbukwa kuwa tayari tawi la vijana la chama cha AfD lilishaorodheshwa kuwa kundi linalofuata itikadi kali wakati chama hicho kilikuwa kikitajwa tu kama mshukiwa wa msimamo huo mwaka 2021.
Soma zaidi:Wabunge wa Ujerumani wataka kuipiga marufuku AfD
Akilizungumzia tangazo la shirika la ujasusi la ndani kuhusu chama hicho, Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Nancy Faeser amesema "AfD inawakilisha dhana ya ubaguzi dhidi ya makundi yote ya watu na kinawatizama raia wenye historia ya uhamiaji kama raia wa daraja la pili."