Shirika la Ujerumani la ujasusi wa ndani limekiainisha rasmi chama cha AfD kuwa cha mrengo mkali na kukieleza kuwa tishio kwa taratibu za kidemokrasia nchini. Uamuzi huo unatoa mamlaka kwa idara husika ya kukimulika chama hicho ikiwa ni pamoja na kuwatumia makachero na mbinu zingine ili kukipeleleza.