AfD na CDU/CDU zachuana katika utafiti wa maoni ya kitaifa
5 Aprili 2025Matangazo
Takriban wiki sita baada ya uchaguzi mkuu, vyama vyote vya CDU/CSU na AfD vilipata 24% katika utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti wa maoni ya INSA kwa niaba ya gazeti la Bild.
Hili ni ongezeko la asilimia moja kwa AfDikilinganishwa na kura ya maoni ya mwisho kama hiyo, na ni matokeo bora zaidi kwa chama hicho kinachoelemea kwenye siasa kali za mrengo wa kulia.
CDU/CSU yapoteza asilimia mbili za kura
Kinyume chake, muungano wa CDU/CSU umepoteza asilimia mbili za kura.
Muungano wa CDU/CSU ulishinda uchaguzi wa bunge uliofanyika Februari 23 kwa asilimia 28.5, lakini hivi karibuni umepoteza uungwaji mkono miongoni mwa wapiga kura.
AfD ilishika nafasi ya pili kwenye uchaguzi huo kwa kuwapata asilimia 20.8.