Utaratibu wa maandalizi ya Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON, unaendelea nchini Morrocco, hii kabla ya kupanga droo katika Ukumbi wa Kitaifa wa Mohammed V mjini Rabat. Timu 24 zilizofuzu zitapangwa katika makundi sita kila moja likiwa na pande nne, huku taifa mwenyeji Morocco likiwekwa kileleni mwa Kundi A. Je, tutarajie nini katika droo ya leo? Luqman Mahmoud mchambuzi wa soka anaeleza.