ADDIS ABABA:Vifo 4 vingine katika mapambano na polisi
5 Novemba 2005Matangazo
Nchini Ethiopia si chini ya watu wanne wengine wameuawa katika mapambano kati ya polisi na waandamanaji.Wafanya maandamano hao wanadai wanachama wa upinzani waliozuiliwa na polisi waachiliwe huru.Tangu wiki moja ya nyuma,dazeni kadhaa ya watu wameuawa na mamia wengine wamejeruhiwa katika mapambano kama hayo.Wapinzani wa serikali wanadai kuwa uchaguzi mkuu uliofanywa mwezi wa Mei ulikuwa na udanganyifu.Na katika matokeo mengine,Umoja wa Afrika umesema kuwa una wasi wasi kwa sababu ya majeshi yaliyoimarishwa kwenye eneo linalozitenganisha Ethiopia na Eritrea.Maafisa wa Umoja wa Mataifa pia mapema wiki hii wamesema wana khofu kuwa vita vipya huenda vikazuka kati ya madola hayo mawili.