You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Abu Bakar al-Baghdadi
Abu Bakar al-Baghdadi ni kiongozi wa kundi la kigaidi linalojiita “Dola la Kiislamu” (IS).
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Ngoma bado nzito Syria
Mapigano makali yalioanza Jumanne jioni na kuendelea usiku kucha katika mkoa wa Latakia, kaskazini magharibi mwa Syria yamesababisha vifo vya watu 39, wakiwemo wanajeshi wa serikali wasiopungua 20.
Obama na Putin wataka mapigano yasimamishwe Syria
Rais Barack Obama wa Marekani na Vladimir Putin wa Urusi wamekubaliana kwamba umwagaji damu nchini Syria lazima ukomeshwe, lakini hawakupendekeza hatua mpya za ufumbuzi wa mgofgoro huo wala kuodosha tafauti zao.
Umoja wa Mataifa wasitisha shughuli za waangalizi wake Syria
Umoja wa Mataiafa umesitisha shuguli za waangalizi wake nchini Syria leo hii kutokana na kupamba moto kwa umwagaji damu wakati vikosi vya serikali vikishambulia kwa mizinga ngome kuu za waasi.
Mkanganyiko wazidi Syria
Wakati mauaji yakiendelea kuripotiwa Syria, Urusi imekana kuhusika kwa namna yoyote kujadili na mataifa mengine juu ya mabadiliko ya uongozi wa juu nchini humo.
Amnesty International: Syria inafanya uhalifu dhidi ya binaadamu
Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limeituhumu Syria kwa kufanya uhalifu dhidi ya binaadamu kwa lengo la kuuzima upinzani.
Maandamano ya Urusi magazetini
Maandamano ya upande wa upinzani nchini Urusi, hali nchini Syria na mgogoro wa fedha katika kanda ya Euro ni miongoni mwa mada zilizohanikiza magazetini hii leo.
Umoja wa Mataifa: Syria imo kwenye vita kamili
Umoja wa Mataifa umesema sasa Syria imo kwenye vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe, huku Marekani ikiilaumu Urusi kwa kuupa utawala wa Rais Bashar al-Assad helikopta za kufanyia mashambulizi.
Mauwaji yashamiri Baghdad
Mashambulio dhidi ya mahujaji wa madhehebu ya shia nchini Iraq yazidi kuuwa watu, huku taarifa zaidi zikisema kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka.
Mashambulizi yazidi nchini Syria
Vikosi vya serikali ya Syria vimeushambulia kwa mizinga mji wa Haffa katika jimbo la kaskazini magharibi la Latakia kwa siku ya nane mfululizo kwa kile kinachoelezwa kama maandalizi ya kuuvamia mji huo.
Mauaji yaendelea nchini Syria
Kiongozi mpya wa upinzani nchini Syria ameutaka Umoja wa Mataifa uchukue hatua madhubuti zinazoweza kutekelezwa kutumia nguvu ili kuwalinda raia kutokana na ukandamizaji unaofanywa na rais wa nchi hiyo, Bashar al Assad.
Wachunguzi wasikia harufu ya miili kuungua
Wachunguzi wa umoja wa mataifa wamesikia harufu ya kuungua kwa miili ya watu na kuona sehemu za miili imesambaa katika kijiji nchini Syria ambako mauaji makubwa yalifanyika. Watu 80, wanaripotiwa kuwa wameuwawa.
Annan aonya Syria kutumbukia vitani
Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu katika mzozo wa Syria Koffi Annan, ameonya kuwa zisipochukuliwa hatua kuushinikiza utawala nchini humo, hali itazidi kuwa mbaya.
Kofi Annan kukutana na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Syria
Mjumbe wa Kimataifa katika mzozo wa Syria, Kofi Annan, leo atawasilisha mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pendekezo la mwisho la kuunusuru mpango wake wa amani unaoelekea kushindwa
Serikali ya Syria yakanusha kufanya mauaji mengine ya maangamizi
Serikali ya Syria imekanusha kufanyika kwa mauaji mengine ya maangamizi katika mkoa wa katikati wa Hama ambako ripoti zinasema kiasi ya watu 100 waliuawa hapo jana.
Syria: Mbinyo wazidi kwa Urusi na China
Urusi imesema kuwa rais Bashar al-Assad anaweza kuondoka madarakani kama sehemu ya suluhisho la kumaliza umwagakaji damu uanaoendelea nchini Syria ,nayo Saudi Arabia imeitaka Urusi kutounga mkono utawala huo ►
Assad akana kuhusika na mauaji ya Houla
Rais Bashar Assad wa Syria ameutetea ukandamizaji wa jeshi lake dhidi ya wapinzani, akisema kwamba daktari anayefanya operesheni ya dharura hawezi kuambiwa ana damu mikononi mwake kwa kujaribu kuyaokoa maisha.
Annan amkazia sauti Assad
Mjumbe wa amani wa kimataifa Kofi Annan ameyashutumu majeshi ya rais wa Syria Bashar al-Assad kwa mauaji pamoja na kuwakamata watu kinyume na sheria .
Hali yazidi kuwa tete Syria
Kiongozi Mkuu wa waasi nchini Syria amemtaka Mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu, Koffi Annan kutangaza kuwa mpango wake umeshindwa.
Syria yahanikiza magazetini
Na kama ada yetu ya kila siku tunakuletea baadhi ya yale waliyoyaandika wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo katika safu zao za maoni.
Walimwengu waishinikiza Syria izuwie damu isimwagike
Mjumbe maalum wa kimataifa kwa Syria,Kofi Annan amemtaka rais Bashar al Assad akomeshe haraka umwagaji damu,huku Marekani na Japan zikijiunga na nchi za magharibi na kuwafukuza mabalozi wa Syria.
Kofi Annan akutana na Assad
Rais Assad wa Syria amekutana na mjumbe maalum wa kimataifa, Kofi Annan, kufuatia mauwaji ya Houla yaliyolaaniwa kimataifa na ambayo serikali ya mjini Damascus inawatupia lawama wanamgambo wa kiislamu.
Annan kwenda Syria haraka
Mjumbe wa Arab League na umoja wa mataifa nchini Syria Kofi Annan anakwenda kwa ziara yake ya pili mjini Damascus akitafuta njia za kuweka uhai katika mpango wake wa amani ,kufuatia mauaji ya kinyama nchini Syria.
SYRIA: vita vya wenyewe kwa wenyewe vyanukia
Mkuu wa ujumbe wa umoja wa mataifa ameonya kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe Syria baada ya wachunguzi hao kuhesabu miili 92, 32 ikiwa ni ya watoto ,katikati ya mji wa Houla kufuatia ripoti za mauaji.
Idadi ya waliouwawa Syria yafikia watu 90
Baraza la Kitaifa la upinzani nchini Syria limeutaka Umoja wa Mataifa kuitisha kikao cha dharura kujadili mauaji ya takriban watu 90 yanayodaiwa kufanywa na vikosi vya serikali katika mji wa Houla Ijumaa (25.06.2012).
Amnesty International yasema UN imeshindwa kuwajibika
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kuonesha ushupavu wake ukilinganishwa na waandamanaji duniani kote.
Ban Ki-Moon ahofia Al-qaeda kuingia Syria
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema anaamini kundi la Al-qaeda lilihusika na mlipuko wa bomu mjini Damascus nchini Syria ambao ulisababisha watu kadhaa kupoteza maisha.
'Majeshi ya Syria yataka kuufuta mji wa Al Rastan'
Majeshi ya serikali nchini Syria yameanza mashambulizi mapya usiku wa kuamkia Alhamis, dhidi ya mkoa wenye upinzani mkubwa wa Homs ambayo yamelenga zaidi mji wa Al-Rastan ulioko mikononi mwa waasi.
Wangaalizi wa amani hatarini Syria
Waangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria wameondolewa katika mji wa Khan Sheikhoun, kaskazini mwa nchi hiyo siku moja baada ya msafara wao kupigwa na kombora katika makabiliano kati ya vikosi vya serikali na waasi.
Syria kwazidi kufukuta
Mapigano makali yametokea siku ya Jumatatu kati ya majeshi tiifu kwa rais Bashar Assad na waasi wa Free Syria katika mji wa al-Rastan ambapo wanajeshi 23 wa serikali wameripotiwa kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Zaidi ya watu 40 wauwawa Syria
Kiasi ya watu 40 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 170 wamejeruhiwa vibaya nchini Syria baada ya kutokea miripuko miwili mikubwa katikati ya jiji la Damascus. Miripuko hiyo pia imeteketeza majengo na magari kadhaa.
Waangalizi wa UN chupuchupu Syria
Kiongozi wa timu ya waangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria aliponea chupuchupu kuuawa baada ya bomu kulipuka karibu kabisaa na msafara wake katika mkoa wa Daraa siku ya Jumatano.
Uchaguzi wapuuziwa na wapinzani Syria
Mataifa makubwa duniani yapo katika jitahada za kudhibiti vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, waangalizi wameripoti vitendo vya mauwaji zaidi vilivyofanywa na vikosi vya usalama vya taifa hilo.
"Uhalifu wa kivita watendeka Syria" - Human Rights Watch
Human Rights Watch imeituhumu Syria kwa uhalifu wa kivita siku chache kabla ya kuanza kwa mpango wa Umoja wa Mataifa kusitisha mapigano, huku mashambulizi yakiripotiwa licha ya mpango huo wa amani unaoelekea kushindwa.
Syria yamlaumu Ban Ki- Moon kwa kupendelea
Syria imemlaumu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki- Moon, kuwa maoni yake yaliyoituhumu serikali ya nchi hiyo kuvuruga mpango wa usitishaji mapigano kuwa ni ya kupendelea.
Marzouk: Assad umekwisha
Rais wa Tunisia, Moncef Marzouk amemshauri rais Bashar Assad wa Syria kuachia madaraka wakati nafasi ya kufanya hivyo bado ipo kwa kuwa kuondoka kwake ni laazima akiwa mzima au mfu.
Baraza la Usalama kuongeza waangalizi wake Syria
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefikia makubaliano juu ya azimio la idadi ya waangalizi nchini Syria, kutoka 30 hadi 300 na kumruhusu Katibu Mkuu wa Umoja huo kuamua hatima ya hilo kutokana na hali.
Umoja wa Ulaya wamuandalia vikwazo vingine Assad
Umoja wa Ulaya umesema umetayarisha vikwazo vipya dhidi ya utawala wa rais Assad, vinavyolenga kuudhoofisha zaidi usiendelee na ukandamizaji.
Clinton ataka Assad abanwe zaidi
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amelitaka Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuiwekea Syria vikwazo vya silaha na kiuchukulia hatua nyingine kali ili kusitisha umwagaji damu unoendelea nchini humo
Umoja wa Mataifa wataka kutuma waangalizi zaidi Syria
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametaka waangalizi zaidi wapelekwe Syria kusimamia utekelezaji wa mpango wa amani uliopendekezwa na Kofi Annan.
Syria yasisitiza itaheshimu mpango wa amani
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Syria, Walid Muallem ambaye yuko ziarani China, amesema nchi yake itaheshimu ahadi iliyoitoa ya kutekeleza mpango wa amani wa mpatanishi wa kimataifa Kofi Annan.
Mpango wa Annan na majaaliwa ya Syria
Licha ya serikali ya rais Bashar al Assad kuukubali mpango wa Koffi Annan, serikali hiyo imeendelea kufanya mashambulizi hasa dhidi ya mji wa Homs ambao ni ngome kuu ya wapinzani wa rais huyo.
Umoja wa Mataifa kutuma waangalizi Syria
Kundi la kwanza la waangalizi wa Umoja wa Mataifa linawasili nchini Syria Jumapili, kusimamia usitishwaji wa mapigano, wakati kuongezeka kwa ghasia nchini humo kukitishia juhudi za kusimamisha umwagaji damu.
Maandamano makubwa yafanyika Syria
Maelfu ya Wasyria leo wameshiriki katika maandamano yaliyoitishwa na wapinzani wa utawala wa rais Bashar al-Assad. Kwa mujibu wa kamati ya uratibu ya kundi la wapinzani, watu watatu waliuwawa katika maandamano ya leo.
Amani ya Syria iko mguu njiani mguu majanini
Ijumaa ya leo (13.04.2012) inatarajiwa kuwa kipimo cha kwanza cha usitishwaji mapigano ulioanza rasmi jana, huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likikutana kujadili upelekwaji wa ujumbe wake nchini Syria.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yavunjwa Syria
Makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Syria yamekiukwa leo baada ya majeshi ya serikali ya Rais Bashar al-Assad kumuuwa raia mmoja wa nchi hiyo katika mji wa Hama uliopo katika eneo la kati la Syria.
Hali ni shwari Syria
Leo ndio siku ambayo mapigano yalipaswa kumalizika Syria, kulingana na mpango wa amani alioupendekeza Kofi Annan. Kuna dalili zinazoonyesha kwamba pande zinazopigana nchini humo zinayafuata makubaliano hayo.
Annan aona uwezekano wa mpango wa amani kutekelezwa
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu nchini Syria, Kofi Annan, leo amesema kwamba bado yapo matumaini kwamba mpango wa amani wa Syria utafuatwa.
Uingereza na Ufaransa zailaumu Syria
Uingereza na Ufaransa zinaishutumu Syria kwa sababu haiufuati mpango wa amani ulioafikiwa. Leo, mapigano makali yaliyouwa watu kadhaa yameripotiwa nchini humo.
Wahariri wanaendelea kulichambua shairi la mabishano
Shairi la Günter Grass na hali nchini Syria na China ni miongoni mwa mada zilizohanikiza magazetini nchini Ujerumani
Muda wa kusimamisha mapigano Syria wamalizika
Kuanzia leo saa 11 alfajiri, umemalizika ule muda wa kuweka chini silaha nchini Syria, kwa mujibu wa mpango wa mjumbe maalum Kofi Annan.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 54 wa 77
Ukurasa unaofuatia