You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Abu Bakar al-Baghdadi
Abu Bakar al-Baghdadi ni kiongozi wa kundi la kigaidi linalojiita “Dola la Kiislamu” (IS).
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Iran yalaani uamuzi wa OIC kuifukuza Syria
Uamuzi wa Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu (OIC) kuisitisha uanachama Syria umelaaniwa na Iran, huku wasiwasi ukitanda kuwa mgogoro wa Syria umevuuka mipaka na Umoja wa Mataifa ukisema watu milioni 2.5 wanahitaji msaada.
Syria yasimamishwa uanachama OIC
Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya ushirikiano wa nchi za Kiislamu, OIC, umeanza katika mji wa Makkaa nchini Saudi Arabia, na unatarajiwa kutangaza kusimamishwa kwa uanachama wa Syria baadaye leo.
Utawala wa Assad waporomoka - Hijab
Aliyekuwa waziri mkuu katika serikali ya Rais Bashar al-Assad wa Syria na ambaye sasa amekimbia nje ya nchi hiyo, amesema utawala wa Assad unaporomoka, licha ya kujijengea picha kwamba bado ni imara.
Waasi wa Syria waidungua ndege ya jeshi la serikali
Waasi nchini Syria wamedai wameidungua ndege ya jeshi la serikali na kumteka rubani wake, huku mapigano yakiwa yanaendelea katika miji ya Damascus na Aleppo. Serikali imesema ndege hiyo ilipata matatizo ya kiufundi.
Syria: Mapigano yaendelea Damascus na Aleppo
Mapigano makali yameripotiwa katika mji mkuu wa Syria Damascus na katika mji wa Aleppo ulio muhimu kibiashara. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanaarifu kwamba majeshi ya serikali yaliongeza mashambulizi.
Syria kupata mpatanishi mpya
Mwanadiplomasia mkongwe na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Algeria Lakhdar Brahimi, anatarajiwa kuwa mpatanishi mpya wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuchukua nafasi iliyoachwa na Kofi Annan.
Syria yapata waziri mkuu mpya
Rais Bashar al-Assad wa Syria amemteua waziri mkuu mpya kuchukua nafasi ya Riad Hijab aliyejitenga na utawala wake wiki hii. Na huko Iran unafanyika mkutano wa kujadili hali ya usalama nchini Syria.
Mkutano juu ya Syria wafanyika Iran
Iran, ambayo ni mshirika wa karibu wa Syria, imeitisha mkutano utakaojadili hali ya usalama ya Syria. Hatua hii inakuja wakati ambapo majeshi ya rais Bashar al-Assad, yakiendelea na mashambulizi dhidi ya waasi.
Uturuki yaionya Iran juu ya Syria
Kila upande unadai kuudhibiti wa mji wa Aleppo, huku mapigano makali yakiendelea kati ya serikali na waasi na Uturuki ikiionya Iran kwa kuihusisha na ghasia za Syria, nayo Iran yenyewe ikiitisha mkutano juu ya Syria.
Iran yakiri wanajeshi wake wastaafu kushikwa mateka Syria
Vifaru vya serikali vimepenya ndani ya maeneo yanayoshikiliwa na waasi mjini Aleppo jambo ambalo limezusha wasiwasi wa makundi ya haki za binaadamu, huku Iran ikikiri wanajeshi wake wastaafu ni miongoni waliotekwa Syria.
Maoni ya wahariri
Wahariri wanatoa maoni juu ya chombo cha anga cha Marekani,"Curiosity" kilichotua kwenye sayari ya Mars. Pia wanatoa maoni juu ya mgogoro wa Syria na mgogoro wa madeni.
Iran na Uturuki zafanya mazungumzo juu ya Syria
Mwakilishi mmoja wa kiongozi wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amefanya ziara ya ghafla nchini Syria kwa ajili ya mazungumzo na Rais Bashar al-Assad katika wakati ambao mapigano nchini humo yanaendelea.
Syria: Waziri mkuu naye aikimbia serikali
Waziri mkuu wa Syria, amejitenga na utawala wa Assad na kukimbilia Jordan usiku wa kuamkia Jumatatu. Msemaji wa waziri huyo amekanusha taarifa ya televisheni ya taifa ya Syria kwamba waziri mkuu alifukuzwa kazi.
Kituo cha televisheni ya taifa chashambuliwa Syria
Mripuko wa bomu umetokea katika jengo la makao makuu ya televisheni ya taifa ya Syria, yaliyopo mjini Damascus. Waziri wa habari wa Syria amesema watu kadhaa wamejeruhiwa lakini hakuna aliyeuwawa.
Waasi washambulia kambi ya jeshi la angani Syria
Huku mapigano yakiendelea kupamba moto nchini Syria rais wa Marekani asemekana kutia saini hati ya siri inayoonesha uungaji mkono wa nchi hiyo kwa waasi wa Syria
Assad awasifu wanajeshi wake
Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema kwamba vita kati ya jeshi la nchi yake na waasi vitaamua hatima ya Syria. Amewapongeza pia wanajeshi wake kwa kupambana na kile alichokiita makundi ya magaidi wahalifu.
Mapambano ya Aleppo yaendelea
Mapambano makali katika mji wa Aleppo, Syria, yanaingia siku yake ya 11 licha ya kuwepo kwa lawama za kimataifa dhidi ya serikali ya nchi hiyo na Umoja wa Mataifa ukisema zaidi ya watu 200,000 wameshaukimbia mji huo.
Vita vya Aleppo vyapamba moto
Mapambano ya kuukamata mji wa Allepo baina ya vikosi vya serikali na waasi yanazidi kupamba moto huko Syria. Waasi sasa wamekiteka kituo muhimu cha ukaguzi kwenye mpaka baina ya nchi hiyo na Uturuki.
Mkataba Mpya wa Kudhibiti silaha wakwamishwa
Mkutano unaojadili rasimu ya mkataba mpya wa kudhibiti silaha uliokwisha Ijumaa umeshindwa kufikia maamuzi juu ya mambo muhimu kuhusiana na biashara hiyo ya mabilioni ya dola.
Marekani, Umoja wa Mataifa wahofia mauaji ya maangamizi Aleppo
Umoja wa Mataifa na Marekani zinasema zinahofia utawala wa Rais Bashar al-Assad unapanga mauaji ya maangamizi katika mji wa kaskazini mwa Syria wa Aleppo wakati vikosi zaidi vya serikali vikitaka kuukomboa mji huo.
Mapigano yaendelea katika mji wa Syria, Aleppo
Waasi nchini Syria wamesema wanadhibiti nusu ya mji wa pili kwa ukubwa nchini humo Aleppo, lakini wanakabiliwa na mashambulizi makali ya wanajeshi watiifu kwa rais Bashar al Assad.
Mapigano yashika kasi Syria
Wanaharakati wa upinzani nchini Syria wanasema mapigano yameshika kasi nchini humo katika maeneo kadha ya mji wa Aleppo, na kufikisha siku ya tano sasa tangu mzozo huo kuingia katika mji huo mkubwa nchini Syria.
Waasi: Hatuko tayari kuunda serikali na mtu wa Assad
Baraza la Kitaifa la Syria limesema halitakubali kuingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa itakayoongozwa na mjumbe wa serikali ya sasa, tafauti na kauli iliyotolewa na mkuu wa baraza hilo asubuhi leo (24 Julai 2012).
Waasi: Syria yapeleka silaha za kemikali mipakani
Waasi wa Syria wanasema serikali imezipeleka silaha za kemikali katika viwanja vya ndege mipakani mwa nchi hiyo, siku moja baada ya utawala kuonya kwamba itazitumia silaha hizo endapo itashambuliwa na mataifa ya kigeni.
Syria itatumia silaha za sumu ikishambuliwa
Syria imekiri leo(23.07.2012) kuwa ina silaha za kemikali na kuonya kuwa itazitumia iwapo itashambuliwa na mataifa ya nje, licha ya kuwa haitazitumia dhidi ya raia wake.
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu: Lazima Assad aondoke
Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Jumuiya ya nchi za kiarabu wamemtolea wito rais Bashar al-Assad kuachia madaraka ili kuepusha umwagaji zaidi wa damu, na kumuahidi njia salama ya kuondokea iwapo atafanya hivyo.
Msiba mmoja baada ya mwingine Syria, maafa yazidi
Waasi wameyashambulia makambi ya wanajaeshi wa serikali mjini Damascus na kuzidisha kizaazaa, kilichodumu kwa siku ya sita mfululizo. Pia, televisheni ya taifa imethibitisha kifo cha mkuu wa ujasusi.
Mgogoro wa Syria mpaka lini?
Shambulizi lililofanyika katika jengo la ulinzi la taifa mjini Damascus ni pigo kubwa kwa mji mkuu huo na kwa uongozi wa Rais Bashar al-Assad, huku wachambuzi wa mambo wakisema huo ni mwisho wa utawala wa Syria.
Urusi, China zalipigia kura ya veto azimio juu ya Syria
Urusi na China kwa pamoja zimelipigia kura ya veto azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililotaka kutumika kwa Ibara ya Saba ya Mkataba wa Umoja huo kuichukulia hatua kali Syria na kusitisha umwagaji damu.
Waziri wa ulinzi wa Syria auawa
Waziri wa ulinzi wa Syria Daoud Rajiha ameuawa katika shambulizi la kujitoa muhanga mjini Damascus. Mji huo pia unagubikwa na mapigano ya siku 4 kati ya jeshi na waasi, huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea.
Udugu wa Kiislamu kuwasaidia wapinzani Syria
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amemwambia mpatanishi wa amani wa mzozo wa Syria, Kofi Annan, kuwa atafanya awezalo kuunga mkono mpango wa Umoja wa nchi za Kiarabu wa kumaliza ghasia Syria.
Msalaba Mwekundu: Yanayotokea Syria ni vita vya wenyewe kwa wenyewe
Shirika la Msalaba Mwekundu sasa linaona mapigano yanayotokea Syria kuwa ni vita vya wenyewe kwa wenyewe huku wataalamu wakisema kuwa hali hiyo inaweza kuwa ni uhalifu wa kivita.
Mapigano yaendelea Syria
Yamezuka mapigano baina ya majeshi ya serikali na waasi katika mji mkuu wa Syria, Damascus. Wanaharakati wanaripoti kwamba mapigano yalitokea pia katika eneo lililo karibu na Ikulu ya rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo.
UN yamnyooshea kidole Assad mauaji ya Treimsa
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na jumuiya ya nchi za kiarabu kwenye mgogoro wa Syria, Koffi Annan ameilaumu serikali ya rais Bashar al-Assad kwa kutumia silaha nzito dhidi ya kijiji cha wakulima cha Treimsa.
Iran yazituhumu Uturuki, Jordan kuwasaidia waasi wa Syria
Wakati serikali na waasi wakilaumiana kwa "mauaji ya maangamizi" katika jimbo la kati la Hama nchini Syria, Iran imezinyooshea kidole Uturuki na Jordan kuwasaidia wapiganaji wanaoipinga serikali ya Bashar al-Assad.
Mauaji mengine ya maangamizi yahofiwa kufanyika Syria
Kuna uwezekano wa mauaji mengine ya maangamizi nchini Syria baada ya miili zaidi ya watu 100 kugunduliwa katikati ya nchi hiyo, huku wanaharakati wakitaka uingiliaji wa mataifa ya Magharibi kuzuia "ukatili wa kinyama".
Balozi wa Syria Irak ajiunga na upinzani
Balozi wa Syria nchini Irak amejitenga na serikali na kujiunga na upinzani. Balozi huyo Nawaf Fares (katikati kwenye picha) anatazamiwa kukutana na viongozi wa Irak leo kuzungumza juu ya kupelekwa katika nchi nyingine.
Juhudi za kidiplomasia kuhusu Syria zapamba moto
Mpatanishi wa kimataifa katika mgogoro wa Syria Kofi Annan atalihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya hatua iliyopigwa kujaribu kusitisha ghasia nchini Syria. Urusi nayo imewaalika wapinzani wa Syria.
Juhudi za amani nchini Syria
Mjumbe wa kimataifa anaesaka ufumbuzi wa mzozo wa Syria,Kofi Annan, yuko ziarani mjini Teheran ambako amepanga kuzungumza na viongozi wa serikali ya Iran -washirika wakubwa wa Syria.
Marafiki wa Syria wakutana Paris
Rais Francois Hollande wa Ufaransa ametaka vikwazo vikali zaidi viwekwe dhidi Rais Bashar al-Assad wa Syria na waasi wa nchi hiyo wapewe ushirikiano zaidi katika kumwondoa Assad madarakani.
China kutohudhuria mkutano wa "Marafiki wa Syria"
China imeungana na Urusi kukataa kuhudhuria mkutano wa kundi linalojiita "Marafiki wa Syria" unaofanyika nchini Ufaransa hapo kesho, huku kukiwa na taarifa za kuongezeka kwa uasi wa wanajeshi nchini Syria.
Wapinzani Syria washindwa kuungana
Wapinzani wa serikali ya Syria wanajaribu kuunganisha juhudi zao katika mkutano unaowaleta pamoja katika mji mkuu wa Misri, Cairo, lakini mgawanyiko baina ya makundi tofauti yao bado unakwamisha juhudi hizo.
Mkutano kuhusu Syria waanza Cairo
Kiasi ya wajumbe 250 wa upinzani wa Syria wanakutana mjini Cairo, Misri, kwenye mkutano wa kuijadili amani ya Syria ulioandaliwa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, lakini waasi na wanaharakati wamepanga kuugomea mkutano huo.
Mataifa makubwa yakubali mpango wa mpito Syria
Mataifa makubwa duniani yamekubaliana Jumamosi (30.06.2012) kuhusu mpango wa mpito nchini Syria ambao unaweza kujumuisha maafisa wa serikali iliyopo madarakani, lakini rais Assad hatahusika katika serikali hiyo.
Annan aelezea matumaini juu ya mkutano wa Syria
Juhudi za kidiplomasia zinaendelea kujaribu kuuokoa mpango wa amani wa Syria siku moja kabla ya mkutano mwingine wa kimataifa ambao unaandaliwa mjini Geneva kutafuta suluhu ya mgogoro uliodumu kwa miezi 16 nchini Syria.
Annan ataka serikali ya mseto Syria
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na jumuiya ya nchi za Kiarabu katika mzozo wa Syria Koffi Annan amependekeza iundwe serikali ya mseto nchini humo ikujumlisha wajumbe kutoka pande zote zinazohasimiana.
Maoni ya wahariri juu ya Rais wa Ujerumani
Wahariri wa magazeti wanazungumzia juu ya maadhimisho ya siku mia moja tokea Joachim Gauck awe Rais wa Ujerumani na pia wanatoa maoni yao juu ya mvutano uliozuka baina ya Uturuki na Syria.
Maoni ya wahariri juu ya ushindi wa Muhammed Mursi
Wahariri wasema Muhammed Mursi atakabiliwa na changamoto kubwa katika kuitekeleza agenda yake kutokana na ukinzani wa wanajeshi.
NATO kujadili kudunguliwa kwa ndege ya Uturuki
Uturuki imeishutumu Syria kwa kuidungua ndege yake ya kivita katika anga ya kimataifa bila onyo na imeitisha mkutano wa jumuiya ya NATO kesho kujadili hatua ya pamoja dhidi ya rais wa Syria, Bashar al Assad.
Wasiwasi kuhusu kudunguliwa ndege ya Uturuki
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu athari za kudunguliwa kwa ndege ya kivita ya Uturuki na Syria.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 53 wa 77
Ukurasa unaofuatia