You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Abu Bakar al-Baghdadi
Abu Bakar al-Baghdadi ni kiongozi wa kundi la kigaidi linalojiita “Dola la Kiislamu” (IS).
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
40 wauwawa Syria
Bomu lililotegwa katika gari nje ya msikiti karibu na mji wa Damascus limewaua watu 40 Ijumaa(25.10.20213),wakati afisa wa Umoja wa Mataifa ameeleza wasi wasi mkubwa kuhusu mamia ya watu ambao wamezingirwa.
Wapiganaji 40 wa upinzani wauwawa Syria
Wanajeshi wa serikali ya Syria leo wamewavamia waasi karibu na mji mkuu, Damascus, na kuwaua wapiganaji wapatao 40 wa upinzani. Mji wa kaskazini wa Safira, kusini mashariki mwa Aleppo, pia umeshambuliwa.
Syria kuwasilisha mpango wa silaha za sumu
Syria inalikabidhi Shirika la Kudhibiti matumizi ya Silaha za Sumu, mpango wa uziteketeza silaha hizo. Wakati serikali ikiwa ikiwaachia huru wafungwa 61 wa kike katika mpango ulioongozwa na Qatar na Palestina
Saudi Arabia yaitahadharisha Marekani
Saudi Arabia imetahadharisha kwamba uhusiano kati yake na Marekani unaweza ukaingia dosari kutokana na jinsi Marekani inavyoendesha sera zake katika kushughulikia mzozo wa Syria na mpango wa nyuklia wa Iran.
Mkutano wa marafiki wa Syria
Mataifa ya Kiarabu na yale ya Magharibi yamekutana mjini London Jumanne (22.10.2013) kuwashinikiza viongozi wa upinzani wa Syria kuhudhuria mazungumzo ya Geneva mwezi ujao kwa kwenda na kauli moja.
Machafuko Iraq yarindima
Nchini Iraq vikosi vya usalama vimetangaza amri ya kutotoka nje katika mji wa Fallujah kufuatia mapigano yaliyozuka katika mji huo.Watu wenye silaha wamepambana na vikosi vya usalama.
Mkutano wa amani Syria utaandaliwa lini?
Hali ya sintofahamu inaonekana kuunzunguka mkutano wa kimataida wenye lengo la kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, kufuatia kauli zinazokinzana juu ya mkutano huo.
Mashtaka mapya dhidi ya walinzi wa Blackwater
Marekani imewafungulia mashtaka mapya ya kuua bila kukusudia walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Blackwater Worldwide kwa mauaji ya mwaka 2007 mjini Baghdad nchini Iraq
Ujerumani yakataa kuwa msuluhishi Syria
Rais Bashar al Assad wa Syria ameitaka Ujerumani kusuluhisha mzozo wa Syria lakini serikali ya Ujerumani moja kwa moja imelikataa wazo hilo ambapo baadhi ya wataalamu wa sera wanaamini kuwa ni uamuzi sahihi.
Putin: Marekani na Urusi zinakubaliana kuhusu Syria
Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema nchi yake na Marekani zinakubaliana juu ya namna ya kuharibu silaha za kemikali za Syria, na kuusifia utawala wa rais Assad kwa kutoa ushirikiano.
Wataalamu wa silaha za sumu kuanza kazi Syria
Wataalamu wa kimataifa wa kuharibu silaha za sumu wanatarajiwa kuanza shughuli ya kuziorodhesha silaha za sumu za Syria kwa kupitia orodha ya maeneo mbalimbali iliyotolewa na serikali ya Syria
Baraza la Usalama laidhinisha azimio kuhusu Syria
Baraza lausalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio jana(27.09.2013)linalotaka kuondolewa kabisa kwa silaha za sumu za Syria lakini halitishii kuchua hatua za kijeshi dhidi ya serikali hiyo iwapo haitatekeleza.
Iran yaridhia kushiriki mazungumzo juu ya silaha za nyuklia
Maafisa wa ngazi ya juu wa Iran na wale wa shirika la UN la kudhibiti matumizi ya nishati ya Atomiki-IAEA, wameanza majadiliano mjini Vienna juu ya uchunguzi wa mpango wa silaha za nyuklia za Iran.
Wataalamu wa Silaha waanza kazi tena Syria
Wataalamu wa silaha wa Umoja wa Mataifa wamerudi katika maeneo ambako inadaiwa yalifanywa mashambulizi ya silaha za kemikali nchini Syria, huku wanadiplomasia wakikaribia muafaka juu ya azimio kwa ajili ya silaha hizo.
Obama hataonana na Rowhani New York
Rais Barack Obama wa Marekani hana mipango ya kukutana na rais wa Iran Hassan Rowhani kujadili mgogoro wa taifa hilo kuhusu mpango wake wa nyuklia, pembezoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Vita vya Syria viko kwenye ''mkwamo''
Naibu waziri Mkuu wa Syria amesema vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini mwake vimefika kwenye mkwamo, na kwamba serikali inaweza kutoa pendekezo la mapatano ya kusimamisha mapigano.
Assad: Orodha ya silaha za sumu yaweza kutolewa ''hata kesho''
Rais Bashar al-Assad wa Syria amesisitiza utayarifu wa serikali yake kukabidhi silaha za kemikali za nchi hiyo, na wakati huo huo akatahadharisha kwamba zoezi la kuziharibu laweza kuchukua muda mrefu, na fedha nyingi.
Ujerumani yawajibika katika Umoja wa mataifa
Mzozo wa Syria na werevu wa Urusi,miaka 40 tangu Ujerumani ilipojiunga na Umoja wa Mataifa na awamu ya mwisho ya kampeni za uchaguzi nchini Ujerumani ni miongoni mwa mada magazetini.
Nchi kubwa zaujadili mswada kuhusu Syria
Wanadiplomasia kutoka nchi tano wanachama wa kudumu wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanakutana mjini New York kujadili mswada wa azimio linalohusu kuteketezwa kwa silaha za sumu za Syria.
Maoni ya wahariri juu ya Syria na uchaguzi wa Ujerumani
Wahariri wanaizungumzia ripoti ya wakaguzi wa Umoja wa Mataifa juu ya kutumiwa silaha za sumu nchini Syria,na pia wanatoa maoni juu ya uchaguzi mkuu wa Ujerumani
Sumu ya Sarin ilitumika Syria
Nchi za magharibi zinatarajiwa kuongeza shinikizo la kupitishwa kwa azimio la umoja wa Mataifa kuishurutisha Syria kuzisalimisha silaha zake za sumu baada ya umoja wa Mataifa kuripoti sarin ilitumika Syria
Jamii ya kimataifa yataka azimio lenye mashiko kuhusu Syria
Ufaransa,Uinegereza na Marekani zinataka azimio la uhakika na lenye mashiko kutoka umoja wa Mataifa kuihusu Syria jinsi itakavyosalimisha silaha zake za sumu kwa jamii ya kimataifa.
Makubaliano kuhusu silaha za Syria yapokelewa vyema
Makubaliano yaliyofikiwa kati ya Marekani na Urusi kuhusu kuteketezwa silaha za kemikali za Syria, yameungwa mkono na nchi nyingi muhimu duniani. Ujerumani, China, Ufaransa na Israel ni miongoni mwa nchi hizo.
Marekani na Urusi zafikia makubaliano ya silaha za Syria
Marekani na Urusi Jumamosi (14.09.2013) zimefikia makubaliano ya kihistoria baada ya mazungumzo ya siku tatu juu ya mpango mkubwa wa kutokomeza silaha za sumu za Syria kufikia kati kati ya mwaka ujao wa 2014.
Ban Ki-moon kubadhiwa ripoti kuhusu Syria
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amesema Ijumaa(13.09.2013) anaamini kutakuwa na ripoti inayoeleza wazi kutoka kwa wakaguzi wa silaha wa Umoja huokuwa silaha za kemikali zilitumika nchini Syria hapo Agosti 21.
Urusi yapongeza hatua ya Syria
Rais wa Urusi, Vladmir Putin amesema hatua ya Syria kujiunga na mkataba wa kimataifa wa kudhibiti matumizi ya silaha za sumu, imedhihirisha imani yake njema na inatoa onyo kali kwa Marekani kutoivamia kijeshi nchi hiyo.
Lavrov na Kerry wakutana kuhusu Syria
Kabla ya mazungumzo ya Geneva rais Assad athibitisha utawala wake uko tayari kuziweka silaha zake za sumu chini ya uangalizi wa kimataifa kwa mujibu wa pendekezo la Urusi na sio kwa vitisho vya Marekani
Urusi yasema amani yawezekana Syria
Sergei Lavrov na John Kerry wanakutana Geneva Uswisi kujadiliana kwa kina kuhusu mpango uliopendekezwa na Urusi katika kuzishughulikia silaha za sumu za utawala wa Assad
Maoni ya wahariri juu ya hotuba ya Obama
Wahariri wanatoa maoni juu ya mgogoro wa Syria na kuchaguliwa kwa Thomas Bach wa Ujerumani kuwa Rais wa Kamati ya kimataifa ya Olimpiki.
Obama aipa fursa diplomasia Syria
Rais wa Marekani Barack Obama amekubali kusitisha kwa muda mpango wa kuishambulia kijeshi Syria, baada ya utawala wa rais Bashar al-Assad kukubaliana na pendekezo la kukusanya na kuharibu silaha zake za kemikali.
Kerry kwa Syria: Kabidhi silaha za sumu uepuke kipigo
Wazi wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, amesema iwapo Syria itakabidhi silaha zake za kemikali, inaweza kuepuka operesheni ya kijashi inayoandaliwa dhidi yake, huku Urusi ikionya mashambulizi yatausambaza ushahidi.
Mkondo mpya katika mzozo wa Syria
Mzozo wa Syria na uwezekano wa kusaka ufumbuzi wa kisiasa pamoja na kampeni za uchaguzi nchini Ujerumani ndizo mada kuu magazetini .
Mpango wa Urusi utaepusha mashambulizi Syria?
Rais wa Marekani Barack Obama ameashiria kuwa atachelewesha kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Syria, iwapo utawala wa Assad utasalimisha silaha zote za Kemikali kwa jumuiya ya kimataifa.
Mzozo wa Syria magazetini
Mzozo wa Syria na Ujerumani kubadilisha msimamo wake dakika ya mwisho,kampeni ya uchaguzi mkuu wa Ujerumani ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa zaidi na wahariri wa magazeti ya Ujerumani.
Marekani kuirejesha Syria katika baraza la usalama...
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry, amesema nchi yake haiondowi uwezekano wa kurudi katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupata suluhisho juu ya Syria, baada ya kukamilika kwa ripoti ya wakaguzi
Hakuna maafikiano kuihusu Syria huku Papa akitangaza siku ya maombi kote duniani
Mkutano wa viongozi wa nchi 20 zinazoongoza kiuchumi duniani, G20 umekamilika jana(06.09.2013) huku viongozi hao wakiwa wametofautiana kuhusu mzozo wa Syria na baba mtakatifu Francis akitoa wito wa maombi ya amani
Viongozi wa G20 wakosa kuafikiana kuihusu Syria
Viongozi wa nchi zenye nguvu zaidi kiuchumi duniani wameshindwa kuafikiana kuhusu mzozo wa Syria katika mkutano unaofanyika nchini Urusi huku Marekani ikitafuta uungwaji mkono kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Syria
Khamenei: Iran kuiunga mkono Syria hadi mwisho
Kiongozi mkuu wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amesema Marekani inayatumia mashambulizi ya kemikali nchini Syria kama kisingizio cha kuivamia nchi hiyo inayokabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Viongozi wa G20 wakutana Urusi
Viongozi wa nchi ishirini zenye uwezo mkubwa kiuchumi wanakutana nchini Urusi kwa mazungumzo yanayonuiwa kuimarisha uchumi wa dunia lakini suala linalotarajiwa kutawala ni mzozo wa Syria
Rais Joachim Gauck nchini Ufaransa
Marais wa Ujerumani Joachim Gauck na wa Ufaransa Francois Hollande wamekitembelea kijiji cha Oradour sur -Glane nchini Ufaransa ambako mafashisti wa kijerumani walifanya mauaji halaiki wakati wa vita kuu vya pili.
Putin aonesha 'kulainika' juu ya Syria
Wakati Marekani ikitarajiwa kuidhinisha hatua za kijeshi dhidi ya utawala wa Syria, Rais Vladimir Putin wa Urusi anaonesha utayarifu wa kuikubali hatua hiyo kama ikithibitishwa serikali ya Assad imetumia silaha za sumu.
Obama aamini Congress itakubali vita vya Syria
Mtaalamu wa kemikali wa serikali ya Syria ameukimbia utawala wa Assad na ushahidi unaothibitisha matumizi ya silaha za kemikali huku Congress ikijadili mipango ya kuivamia Syria kijeshi.
Maoni ya wahariri
Maoni ya wahariri wa magazeti juu ya mgogoro wa Syria na juu ya matatizo ya Ugiriki katika muktadha wa uchaguzi wa Ujerumani.
Wakimbizi wa Syria wafikia milioni 2
Umoja wa Mataifa umesema kwamba vita nchini Syria vimeshawalazimisha raia milioni 2 kuikimbia nchi hiyo na kuwageuza wengine milioni 4 kuwa wakimbizi wa ndani huku Marekani ikiwa inajiandaa kuivamia Syria.
Ufaransa kujadili uingiliaji kati Syria
Kwa mataifa matatu yenye kura ya veto katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa nia yao ni kuishambulia Syria. Lakini inaonekana pia kuwa hali inakwenda kinyume na matakwa yao.
Shambulio lainyemelea Syria
Rais Barack Obama wa Marekani Jumatatu (02.09.2013)anatazamiwa kuimarisha kampeni yake kuwashawishi wabunge wenye mashaka kuunga mkono hatua ya kijeshi dhidi ya Syria wakati nchi ikitaka kuzuiliwa kwa shambuolio hilo.
Obama ataka bunge liamue kuhusu Syria
Kwa muda wa zaidi ya wiki sasa , Ikulu ya Marekani ya White House imekuwa ikielekeza mashambulizi yake kuelekea kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Syria. Lakini hayo yamebadilika rais Obama anataka sasa bunge liamue.
Marekani yasisitiza itaiadhibu Syria
Marekani imedhihirisha wazi kuwa itaiadhibu Syria kwa shambulio la Damascus ambapo zaidi ya watu 1,400 waliuawa huku wachunguzi wa umoja wa Mataifa wakikamilisha uchunguzi wao na kuondoka Syria leo (31.08.2013).
Marekani inapanga kuingilia kijeshi Syria
Marekani inaendelea kusaka "Muungano wa kimataifa" katika maandalizi yake ya kuishambulia Syria ikibidi, kutokana na tuhuma za serikali ya nchi hiyo kutumia gesi ya sumu dhidi ya raia.
Ni lini Marekani itaishambulia Syria?
Rais Barack Obama wa Marekani amesema Jumatano (28.08.2013) bado hajasaini mpango wa kuishambulia Syria lakini kuna uwezekano wa kuchukuliwa hatua hiyo baada ya Marekani kuashiria haitohitaji ruhusa ya Umoja wa Mataifa.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 48 wa 77
Ukurasa unaofuatia