You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Abu Bakar al-Baghdadi
Abu Bakar al-Baghdadi ni kiongozi wa kundi la kigaidi linalojiita “Dola la Kiislamu” (IS).
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Rubani wa Jordan atekwa na IS
Jeshi la Jordan limethibitisha leo kwamba mmoja ya marubani wake ametekwa na kundi la wanamgambo wanaojiita Dola la Kiislamu, IS, baada ya ndege ya rubani huyo kuanguka nchini Syria.
Mwaka 2014 ulikuwa mgumu kwa waandishi wa kimataifa
Kamati ya kimataifa ya kuwalinda waandishi wa habari, CPJ, imesema leo (23.12.2014) waandishi kiasi 60 waliuwawa kazini 2014 au kwa sababu ya kazi yao. Asilimia 44 ya waandishi walilengwa katika mauaji.
Umoja wa Mataifa waomba msaada kwa ajili ya Syria
Umoja wa Mataifa umeomba kiasi cha Dola bilioni 8.4 kwa ajili ya kutoa msaada wa dharura wa kibinaadamu kwa takribani watu milioni 18 wa Syria na kuzunguka ukanda huo unaokumbwa na mzozo.
Peshmerga wawajeresha nyuma IS
Operesheni ya siku mbili ya kijeshi ya wapiganaji wa Peshmerga katika jimbo la Kurdistan imefanikiwa kufungua njia kuelekea Mlima Sinjar, uliokuwa umezingirwa na kundi lijiitalo Dola la Kiislamu.
Maoni ya wahariri juu ya Cuba na Marakeni
Wahariri wa magazeti ya Ujerumani katika kurasa zao za maoni leo wanazungumzia juu ya uhusiano baina ya Cuba na Marekani na juu ya uamuzi wa Ujerumani wa kuwapeleka askari wake kaskazini mwa Irak
Marekani yapitisha bajeti kubwa ya kijeshi
Baraza la seneti la Marekani limeidhinisha zaidi ya dola nusu trilioni kwa matumizi ya kijeshi siku ya Ijumaa. (12.12.2014) Mabilioni kadhaa ya fedha hizo zimetengwa makhususi kupambana na kundi la Dola la Kiislamu, IS.
Mogherini ziarani Uturuki
Mkuu mpya wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini kukutana na viongozi wa Uturuki kwa mazungumzo yanayotarajiwa kulenga vita dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu nchini Syria
Israel yatuhumiwa kuihujumu Syria
Syria inaituhumu Israel kufanya mashambulio mawili ya angani dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na serikali karibu na mji mkuu Damascus,ikidai Israel "inawaunga mkono moja kwa moja" waasi na wanamgambo wa itikadi kali.
Mawaziri wakutana Brussels kujadili kitisho cha IS
Mawaziri kutoka takriban nchi sitini walio katika muungano wa kupambana kijeshi dhidi ya wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi la Dola la Kiislamu IS wanakutana hii leo kwa mkutano wa ngazi ya juu mjini Brussels
Papa Francis yuko ziarani Uturuki
Kiongozi wa kanisa Katoliki ulimwenguni, Papa Francis anaanza ziara ya siku tatu nchini Uturuki, lengo likiwa kuhimiza maridhiano kati ya waumini wa kanisa Katoliki wa waumini wa madhebu ya Orthodox.
Mashambulizi ya Syria Raqqa yauwa raia 95
Mashambulizi ya jeshi la Syria yaliyofanywa siku ya Jumanne kwenye ngome ya kundi la Dola la Kiislamu mjini Raqqa yamewauwa watu 95 na kuharibu miundombinu, huku wawili wakishtakiwa Marekani kwa kuiunga mkono IS.
Marekani kuwapeleka wanajeshi zaidi Iraq
Marekani itatuma wanajeshi zaidi kwenye kampeni dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu, huku jitihada za kimataifa dhidi ya kundi hilo zikiendelea. Ufaransa imesema vijana wengi wanajiunga kwenye makundi ya siasa kali.
Wakurdi wafanya operesheni mpya dhidi ya Dola la Kiislamu
Wapiganaji wa Kikurdi na wanajeshi wa serikali ya Iraq wamefanya mashambulizi mapya jana (19.11.2014) katika maeneo yaliyotekwa na wanamgambo wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS nchini humo.
Usalama waimarishwa siku ya Ashura
Maelfu ya waumini wa madhehebu ya Shia nchini Iraq wamekusanyika kwenye mji mtakatifu wa Karbala kwa ajili ya kushiriki Ashura kukumbuka mauaji ya Imam Hussein,mjukuu wa mtume Mohammad
Usalama waimarishwa Iraq
Iraq imeimarisha usalama huku kukiwa na hofu ya kundi la Dola la Kiislamu kufanya mashambulizi makubwa wakati Waishia Jumatatu (03.11.2014) wakikusanyika katika mji wa Karbala.
Mauaji ya wakimbizi Syria
Marekani imefadhaishwa na ripoti kwamba serikali ya Syria imedondosha mabomu ya mapipa kwenye kambi ya wakimbizi katika mji wa Idlib na kuliita shambulio hilo kuwa mauaji makubwa ya kinyama
Wapiganaji wa Peshmerga waelekea Kobane kupambana na IS
Wapiganaji wa kikurdi wa Iraq wanaojulikana kama Peshmerga wamewasili mapema leo asubuhi kusini mashariki mwa Uturuki tayari kuelekea mjini Kobane nchini Syria kuwasaidia wakurdi wenzao kupambana na wanamgambo wa IS
Maoni:Mkutano kuhusu Syria usio na umuhimu?
Mkutano kuhusu wakimbizi wa Syria uliofanyika Berlin haukuhusu utoaji wa ahadi za kifedha, lakini katika maoni yake mwandishi wa DW Dagmer Engel anatoa sababu kumi kwa nini mkutano huo ungeweza kuwa na umuhimu.
IS yazidi kupigana licha ya mashambulizi dhidi yake
Ushirika unaoongozwa na Marekani umeendeleza mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la IS ndani ya Syria na Irak, huku ushirika huo ukinuia kulipiga vita kundi hilo kupitia mtandao wa Intaneti linaoutumia kuvutia wafuasi.
Maandamano ya Cologne na uchaguzi wa Ukraine magazetini
Maandamano ya mjini Cologne yaliyoitishwa na makundi ya wafanyafujo au Hooligans wakishirikiana na wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia na matokeo ya uchaguzi nchini Ukraine ni miongoni mwa mada magazetini
Wakurdi wa Iraq kutuma silaha Kobane
Siku 40 zimepita tangu waasi wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu waanze kushambulia mji wa Kobane uliopo Kaskazini mwa Syria. Hata hivyo wakurdi wa Iraq hawatatuma wapiganaji Kobane kuwasaidia wenzao.
Marekani yasema IS imezuiwa
Marekani inasema harakati za IS zimezuiwa na mashambulizi ya anga yanayoongozwa na jeshi lake ambayo yameshauwa zaidi ya wanamgambo 500, ingawa taarifa zinaonesha kundi hilo linaendelea kujiimarisha.
Walinzi wa Blackwater wakutwa na hatia
Mahakama moja ya jijini Washington, Marekani imewakuta na hatia walinzi wanne wa kampuni ya Blackwater. Mwaka 2007, walinzi hao waliwaua kwa kuwapiga risasi raia wa kawaida wasiopungua 14 nchini Iraq.
Juncker atakiwa kuleta mabadiliko
Wahariri wanaijadili kamisheni mpya ya Umoja wa Ulaya inayoongozwa na Jean-Claude Juncker. Mada nyingine ni vijana kutoka nchi za Magharibi wanaojiunga na kundi la Dola la Kiislamu Iraq na Syria.
Waziri Kerry ziarani Ujerumani
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry atazungumza na maafisa wa Ujerumani kuhusu mapambano dhidi ya wanamgambo wa kundi la Dola la kiislamu, ugonjwa hatari wa Ebola na mpango wa nyuklia wa Iran.
Kurdistan kupeleka wapiganaji Kobane
Bunge la Kurdistan linapiga kura kuviruhusu vikosi vyake kwenda Syria kuwasaidia Wakurdi wanaopambana na wapiganaji wa Dola la Kiislamu, huku mapambano makali yakiendelea mjini Kobane na vitongoji vyake.
Uturuki yatakiwa kuchukua hatua dhidi ya IS
Habari moja inayozungumziwa magazetini ni mapambano kati ya Dola la Kiislamu na wapiganaji wa Kikurdi katika mji wa Kobane. Wahariri wamegusia pia mjadala wa kiuchumi kati ya ujerumani na Ufaransa.
Wakurdi waendelea na mapambano dhidi ya IS -Kobane
Wapiganaji wa kikurdi katika mji wa Kobane nchini Syria wanaendelea kupambana vikali na wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi linalojiita dola la kiislamu IS huku wakisubiri kupigwa jeki na wenzao kutoka Iraq
Marekani yawadondoshea silaha Wakurdi
Jeshi la Marekani limedondosha silaha, masanduku ya risasi na vifaa vya matibabu kwa Wakurdi wanaopigana na wanamgambo wa Dola la Kiislamu - IS mjini Kobane katika mpaka wa Syria
Mapigano dhidi ya Wanamgambo wa IS yapamba Moto
Wapiganaji wa kikurdi wakisaidiwa na hujuma za ndege za kivita za nchi shirika zinazoongozwa wanaendelea kupambana na wanamgambo wa itikadi kali wa dola la kiislam katika mji wa Kobane wa Syria unaopakana na Uturuki.
Wanamgambo wa itikadi kali wa IS wabanwa Kobane
Marekani inasema imewauwa "mamia kadhaa" ya wanamgambo wa itikadi kali wa dola la Kiislam IS katika mji wa Kobane, ingawa inakiri mji huo unaweza kuangukia mikononi mwa waasi hao wanaosonga mbele pia nchini Iraq.
Hatma ya Kobani yamtia mashaka Obama
Rais wa Marekani Barack Obama amesema vita dhidi ya kundi la Dola ya Kiislamu IS vinaweza kuchukuwa muda mrefu, na kueleza wasiwasi juu ya namna wapiganaji hao wanavyosonga mbele kwa haraka nchini Iraq na Syria.
Wakuu wa majeshi mataifa 22 kuijadili IS
Makamanda wa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani dhidi ya Dola ya Kiislamu wanakutana Washington leo hii kwa lengo la kujadili namna ya kudhibiti kusonga mbele kwa wapiganaji wa kundi hilo.
Uturuki yakubali kujiunga na mapambano dhidi ya IS
Uturuki imeikubalia Marekani kutumia kambi zake za kijeshi kufanya mashambulizi ya angani dhidi ya wanamgambo wenye itikadi kali wa dola la kiislamu- IS huku wapiganaji wa kikurdi wakiendelea kupambana na waasi wa IS
Marekani yakiri mapambano ya mjini Kobani ni magumu
Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel amesema siku ya Jumamosi kuwa mji wa Syria wa Kobani ni tatizo kubwa na gumu, lakini mashambulizi ya angani yamepiga hatua katika kuwarudisha nyuma wapiganaji wa Dola ya Kiislamu.
Mapambano yanaendelea kuudhibiti Kobane
Jopo la wanajeshi wa Marekani na Uturuki watakutana wiki ijayo mjini Ankara kujadili mapigano dhidi ya wanamgambo wa IS baada ya Marekani kuibinya Uturuki kujiunga na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani.
Uturuki yasema haiwezi kupigana peke yake nchini Syria
Uturuki leo imeyaambia mataifa ya magharibi kuwa haiwezi kutarajiwa kuongoza peke yake operesheni ya kijeshi ya ardhini dhidi ya wapiganaji wa jihadi nchini Syria.
Uturuki, NATO na Marekani zakutana kuhusu IS
Wanamgambo wa Dola la Kiislamu leo wamechukua thuluthi moja ya eneo la mji muhimu wa mpakani nchini Syria, Kobane, wakati Uturuki ikikataa kuyatuma majeshi yake kwenda kupambana na wapiganaji hao wa jihadi.
Mashambulizi mapya kwa IS yafanyika Kobane
Ndege moja ya muungano wa Kimataifa unaoongozwa na Marekani unaopambana na wanamgambo wa dola la kiislamu IS, imefanya mashambulizi mapya ya angani ikiyalenga maeneo ya mji wa Syria unaopakana na Uturuki wa Kobane.
Kobane wakaribia kuangukia mikononi mwa kundi la IS
Wapiganaji wa Jihad wako ukingoni mwa kuukamata mji wa mpakani wa Syria wa Kobane, wakati Uturuki ikionya kuwa baada ya mashambulizi ya wiki tatu ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu mamia ya watu wameuwawa.
Waislamu watakiwa kulaani kundi la Dola la Kiislamu
Waislamu nchini Ujerumani wanavyochukua hatua dhidi ya wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu , mjadala juu ya kulijenga upya jeshi la Ujerumani, na mkutano wa maaskofu wa kanisa Katoliki.
Wakurdi wapambana na IS mjini Kobane
Wanamgambo wa Dola la Kiislamu wanakaribia kuukamata mji muhimu wa Syria, Kobane, katika mpaka wa Uturuki, baada ya kuzitwaa wilaya tatu za mashariki mwa mji huo kufuatia makabiliano makali na wapiganaji wa Kikuurdi
Baraza la Usalama lalaani mauaji ya Henning
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vidio mpya inayoonesha kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) likimkata kichwa mateka wa Kiingereza, Alan Henning, likisema mauaji hayo ni 'woga'.
IS yaukaribia mji wa Kobani
Mapigano makali yameripotiwa leo kati ya wanamgambo wa kikurdi na wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS katika mji uliozingirwa karibu na mpaka baina ya Uturuki na Syria.
Uturuki kujiunga na operesheni dhidi ya IS
Bunge la Uturuki linatarajiwa kuupigia kura muswaada utakaotoa mamlaka kwa serikali mpya kufanya uvamizi wa kijeshi nchini Syria na Iraq. Hayo yanajiri wakati mashambulizi yakiendelea katika moaka wa Syria na Iraq
Wanamgambo wa IS waandamwa na vikosi shirika vikisaidiwa na wakurd
Nchi za ushirika unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la wanamgambo linalojiita Dola la Kiislamu, IS, zimefanya mashambulizi kaskazini ya Syria zikisaidiwa na vikosi vya Wakurdi katika mji wa Ain al-Arab
Netanyahu aishambulia Iran, Hamas na IS
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema katika Umoja wa Mataifa, kwamba Iran iliyo na silaha za nyuklia ni kitisho kikubwa kwa amani ya dunia kuliko kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS.
Obama: Tulikadiria vibaya uwezo wa IS
Rais wa Marekani Barack Obama amesema nchi yake ilikisia vibaya nguvu za kundi la IS, na uwezo wa jeshi la Irak kukabiliana na kundi hilo. Wakati huo huo mashambulizi yameendelea dhidi ya kundi hilo
Marekani yaendeleza mashambulizi dhidi ya IS
Muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la dola la kiislamu IS umefanya mashambulizi mapya ya kutokea angani dhidi ya kundi hilo nchini Syria, yaliyolenga viwanda vya mafuta kwa siku ya pili
Mashambulizi ya Marekani yauwa watu 19 Syria
Karibu watu 20 wameuwawa wakiwemo wapiganaji 14 wa itikadi kali na raia watano kufuatia mashambulizi ya anga yanayoongozwa na Marekani dhidi ya kundi linalojiita Dola ya Kiislamu, IS, huko mashariki mwa Syria.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 44 wa 77
Ukurasa unaofuatia