ABIDJAN : Waandamana kwa vurugu juu ya taka za sumu
16 Septemba 2006Mamia ya wanadamanaji wenye hasira mjini Abidjan wamefanya ghasia hapo jana kuhusiana na kashfa ya taka za sumu nchini Ivory Coast ambayo imegharimu maisha ya watu saba na kusababisha wengine maelfu kuuguwa pamoja na kujiuzulu kwa serikali ya nchi hiyo.
Licha ya kutangazwa na Waziri Mkuu Charles Konan kwamba usafishaji wa taka hizo za sumu zilizotupwa mjini humo kinyume na sheria utaanza hapo Jumapili wakaazi wanaofikia 300 wa mji huo wameadamana kwa fujo kuonyesha kutoridhika kwao baada ya kuvuta harufu mpya mbaya kutoka kwenye taka hizo katika mjio huo mkuu wa kiuchumi wa Ivory Coast.
Waziri wa Uchukuzi Innocent Anaky Kobeman aliburuzwa kwa kutolewa nje ya gari lake na wakaazi hao ambao walimlazimisha avute harufu hiyo mbaya ya taka za sumu zilizotupwa mjini humo mwezi mmoja uliopita.
Baadae gari lake lilitiwa moto na waziri huyo ilibidi aondolewe kwa kutumia helikopta kutoka mjini humo.