ABIDJAN: Mamia ya vijana walipambana na askari polisi, na baadaye ...
4 Desemba 2003Matangazo
wakafanya mgomo wa kukaa kitako nje ya kituo cha kijeshi cha Kifaransa nchini Ivory Coast, ikiingia siku ya tatu ya maandamano yalioutikisa mji mkuu Abidjan. Vijana wanataka askari kama elfu 4 wa kifaransa kuondoka kwenye eneo la usitishaji mapigano linalotenganisha sehemu ya kaskazini inayodhibitiwa na waasi, na ya kusini iikikaliwa na majeshi ya serikali. Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Michelle Alliot-Marie alitamka majeshi ya kifaransa yatasalia huko kusimamia jinsi muwafaka wa usitishaji mapigano unavyotekelezwa baina ya vikosi vya serikali na waasi.